Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson
Msigwa ilmeeleza kuwa Rais Magufuli amesaini sheria hiyo jana tarehe 16
Novemba 2016 na kuwapongeza wadau wote kwa kufanikisha kutungwa kwake.
Novemba 4 mwaka huu Rais Magufuli katika mkutano wake na wahariri wa
vyombo vya habari nchini alisema kuwa mara tu sheria hiyo
itakapofikishwa kwake ataisaini mara moja.
Rais Magufuli alisema hayo huku kukiwa na malalamiko kutoka kwa wadau wa
habari nchini wakiomba muda kupitia sheria hiyo na kutoa maoni yao.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT