Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe.
Moshi. Chadema imeunda kikosi kilichopewa jina la G5 Jimbo la Moshi Mjini ili kujihakikishia ushindi katika Uchaguzi Mkuu wa 2020.
Kikosi hicho kimepewa jukumu la kusajili wanachama na kuwapatiwa kadi
mpya za uanachama za kielektroniki, ambazo zina uwezo wa kuhifadhi
taarifa zote.
Katibu wa Chadema Mkoa wa Kilimanjaro, Basil Lema aliliambia gazeti hili
jana kuwa, kikosi hicho kiliundwa juzi baada ya kupitia mafunzo maalumu
yaliyowapiga msasa madiwani na wajumbe.
Source: Mwananchi
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT