Mshauri na msemaji wa rais wa Burundi Willy Nyamitwe amenusurika kuuawa
na watu ambao bado hawajajulikana katika shambulizi walililoendesha
usiku wa Jumatatu kuamkia Jumanne.
Shambulizi hilo limeendeshwa na watu waliokuwa na sinaha wakati ambapo
Willy Nyamitwe alikuwa akirejea nyumbani kwake Kajaga Magharibi mwa
Bujumbura.
Katika shambulizi hilo la kuvamia polisi mmoja amemaliziwa maisha.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na waziri wa habari Nestor
Bankumukunzi ni kwamba Willy Nyamitwe alijeruhiwa mkononi na kupelekwa
hospitali.
Kwa upande wake Willy Nyamitwe ametoa shukrani kwa wote waliomtakia
afueni na kusikitishwa na kifo cha mmoja miongozi mwa walinzi wake.
Willy Nyamitwe ni miongoni mwa viongozi waliokuwa mstari wa mbele
kufahamisha kuwa rais Nkurunziza anayo haki ya kuwania kiti cha urais
katika muhula wa 3 mwaka 2015.
Hali ya usalama nchini Burundi imeyumba tangu kutangazwa kwa rais Nkurunziza kuwania kiti cha urais mwaka 2015.
Watu zaidi ya 500 wamekwisha fariki kutokana na ghasia na wengine 310 000 kulazimika kuikimbia nchi.
Ripoti hiyo ilitolewa na shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu mwanzoni mwa mwezi Novemba.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT