Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Juma Mahadhi, amefunguka kwamba amechoshwa
na maisha ya kukaa benchi katika kikosi hicho na katika mzunguko huu wa
pili anajifua vilivyo kuhakikisha anaingia katika kikosi cha kwanza.
Mahadhi aliyejiunga na Yanga mwanzoni mwa msimu huu akitokea Coastal
Union ya Tanga, amekumbana na ushindani mkubwa mbele ya viungo wenzake
Simon Msuva na Geofrey Mwashiuya jambo ambalo linasababisha atumike kama
chaguo la mwisho mbele ya nyota hao.
Akionyesha kujiamini, Mahadhi amesema ameamua kuja kitofauti kwa ajili
ya kujihakikishia namba ya kuanza kwenye kikosi cha kwanza cha Mzambia,
George Lwandamina ambapo atajitahidi kuongeza juhudi ili kupata nafasi
hiyo.
“Sasa hali ya kutocheza mara kwa mara imenichosha kwani nahitaji nafasi
ya kuonyesha mchango wangu kwenye timu ambapo nimepanga katika mzunguko
huu wa pili nijifue zaidi kwa ajili ya kuliaminisha benchi la ufundi na
wanipe nafasi hiyo.
“Najua kwamba haitakuwa kazi rahisi kwani ninaoshindana nao ni watu
wenye viwango vikubwa kama mimi lakini hilo halitanifanya nikate tamaa
kwani lengo langu ni kuona nacheza mara kwa mara,” alisema Mahadhi.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT