Miaka 30 jela kwa jaribio kubaka mtoto | Bepari Classic
Breaking News
Loading...

Alhamisi, 24 Novemba 2016

Miaka 30 jela kwa jaribio kubaka mtoto

MAHAKAMA ya Wilaya ya Kongwa, mkoani Dodoma imemhukumu mkazi wa kijiji cha Mkoka, Lazaro Madeha (56), kutumia kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kutaka kumbaka mtoto wa miaka tisa.


Hukumu hiyo ilitolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Mary Senapee, baada ya kumtia hatiani kwa kosa hilo alilotenda Juni 26, mwaka huu, saa 12.30 jioni katika kijiji cha Mkoka, wilayani humo.

Katika kesi hiyo ilidaiwa Madeha alijaribu kutaka kumfanyia mtoto huyo kitendo hicho baada ya kumuingiza chumbani kwake.

Ilidaiwa mtuhumiwa alimkamata kwa nguvu mtoto huyo ambaye ni wa kambo na kumwingiza chumbani kwake kisha kumvua nguo zote kwa nia ya kujaribu kumbaka.

Hakimu Senapee alidai mtuhumiwa alitenda kosa hilo huku akijua ni kinyume cha sheria, kwani alimuingiza chumbani kwake na kumvua nguo zote na kisha na yeye kuvua nguo kwa lengo la kutekeleza nia ovu.

“Alifanya kitendo hicho wakati mama wa mtoto akiwa kisimani kuchota maji, aliporejea alimkuta mtuhumiwa akiwa mtupu pamoja na mtoto wake kitandani, hali iliyomshtua na kuanza kupiga yowe hadi majirani walipofanikisha kumkamata huku akiwa mtupu,” alisema.

Share this

Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT