Habari yako mpenzi msomaji wa blog yetu. Nina hakika unaendelea vyema. Kwa upande wangu niko sawasawa na ndiyo maana leo tena naendelea kukuletea makala mbalimbali ambazo ni yangu matumaini hazitokuacha vile vile ulivyokuwa awali bali zitaleta mchango mkubwa katika maisha yako. Na ninakuahidi utafikia mafanikio au ndoto kubwa bila kikwazo chochote.
Mpenzi msomaji wetu, leo nimekuletea tabia kumi ambazo zinatoa hakikisho la kufa masikini na kutokufikia mafanikio au ndoto kubwa. Kama wewe ni sehemu ya tabia hizi, rai yangu kwako ni kuchukua hatua mara moja. Badilika. Tabia hizi ni lazima zitaendelea kukufanya kuwa na maisha magumu kadri siku zinavyoenda. Itafika wakati Utaona wingu kubwa na zito kuelekea ndoto zako. Utaanza kusubiria ndugu au jamaa kuja kutatua matatizo yako au kusubiria siku moja kukutana na zali/bahati ya mtende ili kufikia ndoto kubwa. Kama mawazo yako yanasubiria hayo nikwambie huna tofauti na anaengojea embe dodo kuanguka chini ya mti wa muarobaini.
Tabia hizi ukichunguza kwa umakini ni tabia za watu wengi wanaokuzunguka. Pamoja na kuwa na tabia hizi ambazo ni kikwazo kikubwa cha mafanikio yao lakini bado wanaamini watafikia ndoto kubwa au mafanikio makubwa bila ya kuchukua hatua ya kubadilika.Nakuhakikishia Kufikia mafanikio au furaha ya kudumu ni ndoto kamahutochukua hatua. Kama hujui mchawi wako wa kufikia malengo yako basi tambua kuanzia sasa ni tabia hizi hapa:-
1. Kama hufanyi maamuzi. Suala la kufanya maamuzi juu ya mambo ya kufanya au jambo gani hulihitaji na lipi unalihitaji kwa wakati husika ni muhimu sana katika safari ya mafanikio. Usipokuwa na maamuzi yako na kuendekeza kumfurahisha kila mmoja mbele yako ni waziumeshakata shauri la kushindwa kwenye kila jambo maishani mwako. Utamfurahisha kila mtu na hatimaye wewe utajikuta hakuna jambo la msingi umelifanya kwa ajili ya maisha yako ya sasa na ya baadae. Na umri wazidi kusogea vya kutosha, utaanza kuona umechelewa katika kila jambo lolote utakaloshika, na hatimaye nikukaa tamaa kabisa.Hapo umasikini utakusonga kila sehemu ya mwili wako.
2. Kama hufanyi mabadiliko. Mabadiliko ni dhana muhimu sana katika safari ya mafanikio. Bila mabadiliko ni ngumu kuingia kwenye hatua nyingine ya kimaisha ambayo ni bora zaidi ya awali. Mabadiliko huruhusu mafanikio kushamiri na kudumu zaidi katika kiwango cha juu zaidi. Kama hufanyi mabadiliko ni lazima utaendelea kuwa kwenye hali hiyo hiyo ulionayo leo au siku zote. Kama hubadili namna unavyofikiri, unavyowaza; kama hutobadili mitizamo na tabia yako ni wazi utaendelea kubaki ulipo na hatimaye utabaki kusimulia wenzio mafanikio ya wengine. Na utakuwa umekata tiketi ya kudumu ya basi la umasikini.
3. Kuhairisha mambo (Procrastination). Hii ni tabia bingwa kwa wasio na mafanikio wengi.Tabia hii inatoa hakikisho la kuendelea kuwa masikini na kuendelea kuishi maisha ya wastani (mediocre) daima. Tabia hii ya kuahirisha mambo inapoendelea kufanywa kila mara huzidi kukomaa na kujikuta unahairisha hadi mambo ya msingi. Kila jambo jema unalotaka kulifanya unalipiga tarehena visingizio kibao. Huanzi biashara unasubiria siku mambo yawe sawa zaidi, unahairisha. Huanzi kusoma vitabu unasema nitaanza, unahairisha. Huachi tabia hasi zinazokuzuia kusonga kufika ndoto kubwa, unahairisha. Yaani wewe nikuhairisha tu kila kitu badala ya kuanza sasa hivi. Kwa mwendo huu nakuakikishia lazima uendelee kulia maisha magumu serikali imetutupa.Kama umechagua kushindwaendelea na tabia hii na utafika salama salimini.
4. Kutokujisomea vitabu.Ukichunguza wanamafanikio wote duniani wanatabia moja ya kufanana. Tabia ya kutafuta maarifa zaidi. Lakini wengi wenye ndoto ya kufikia mafanikio makubwa katika jamii yetu hawasomi vitabu kabisa.Wamemaliza shule au chuo basi kujisomea imekuwa ni adhabu kwao. Nikwambie kwa taarifa yako ni maarifa madogo sana umepata ukiwa shuleni kwa ajili ya kukufikisha kwenye kilele cha mafanikio makubwa au ndoto zako. Zaidi shuleni umejifunza misingi ya kuzidi kutafuta maarifa. Endelea kutosoma vitabu na kutafuta maarifa, maana unazidi kujiweka mahali pazuri pa kutofikia mafanikio makubwa. Kutopenda kusoma kutakusaidia kushindwa kufanya mabadiliko, kubadili tabia na kukunyima kuona fursa mbalimbali zinazokuzunguka.
Itaendelea tena kesho katika mfululizo wa pili wa tabia hizi.usikose. Endelea kutembelea mtandao wetu
Ukijenga utamaduni wa kutembelea mtandao huu kila siku muda si mrefu unakuwa tajiri wa mali, maarifa na afya. Kazi kwako!
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT