Dalili Tatu(3) Kwamba Biashara Yako Inahitaji Mabadiliko Ya Haraka. | Bepari Classic
Breaking News
Loading...

Jumamosi, 12 Novemba 2016

Dalili Tatu(3) Kwamba Biashara Yako Inahitaji Mabadiliko Ya Haraka.

Ni siku nyingine tumekutana hapa darasa letu la BEPARI CLASSIC kupeana ushauri na mbinu mbali mbali za kufanikisha kufanikwa katika biashara. Siku ya leo nakuletea Dalili Tatu(3) Kwamba Biashara Yako Inahitaji Mabadiliko Ya Haraka. Karibu tuungane.Image result for biashara
Biashara inapokwenda vizuri ni rahisi sana kukosa umakini na kuendesha biashara kwa mazoea. Hapa unakuwa huna presha yoyote kwa sababu biashara inaenda kwa faida na changamoto sio hatari sana kwa biashara yako.
Hii ni hali ambayo wafanyabiashara huwa tunaifurahia sana kwenye biashara zetu. Lakini pia ni hali hatari sana kwa biashara yako kwa sababu kadiri unavyoendesha biashara yako kwa mazoea ndivyo unavyoiweka kwenye hatari ya kushindwa.
Biashara nyingi ambazo zinakufa, huwa hazifi mara moja, yaani leo biashara yako iko vizuri sana halafu ghafla kesho imekufa, haijawahi kutokea hivi. Kabla biashara yako haijafikia kufa, kuna dalili nyingi sana ambazo huwa zinaonekana. Ukiwa mfanyabiashara makini na kufanyia kazi dalili hizo utaweza kuikoa biashara yako isifikie hatua ya kufa kabisa.

Kwa sababu kazi kubwa ya mtandao huu NAPENDA BIASHARA ni kukufanya wewe kuwa mfanyabiashara makini, leo tunakushirikisha dalili tatu kubwa ambazo ukiziona unatakiwa kuchukua hatua haraka kwenye biashara yako.
Zijue dalili hizi na mara zote ziangalie kwenye biashara yako ili iendelee kukua na kukuletea faida kubwa.

Dalili ya kwanza; ukuaji wa biashara sio wa kuridhisha.
Biashara huwa zinapitia vipindi tofauti, kuna wakati biashara inakuwa na kuna wakati inashuka, kupanda na kushuka ni jambo la kawaida. Ila kama biashara inaelekea kushuka tu bila kupanda, stuka haraka kuna tatizo linaendelea.
Kwa kawaida tunategemea biashara iwe inasonga mbele, mauzo yanaongezeka kadiri siku zinakwenda, wateja wanaongezeka na hata mtaji wa biashara unaongezeka. Sasa kama kila unapofanya tathmini unaona biashara inaelekea kushuka, ni vyema ukaanza kuchunguza haraka chanzo cha tatizo hilo ni nini na kuanza kuchukua hatua haraka.
Dalili ya pili; washindani uliowaona ni wadogo wanakuja kwa kasi.
Japokuwa lengo lako kubwa kwenye biashara sio kuhakikisha unamshinda mshindani wako, bado unahitaji kujua hali ya soko ikoje. Unapoingia kwenye biashara na ukaweka juhudi kiasi kwamba wewe ndio ukawa namba moja kwenye soko, unakaribisha watu wengine kuingia kwenye biashara hiyo pia. Na tena wengi watakuwa wanafanya kwa mbinu unazotumia wewe. Sasa kama utajisahau na kuona tayari wewe upo juu, unaweza kushangaa washindani wako wanakuja kwa kasi na tayari wamechukua wateja wengi kutoka kwako.
Unapoona hali hii ni wakati wa kufanya mabadiliko haraka kabla washindani hawa hawajakuondoa kabisa kwenye soko.
http://beparilakihaya.blogspot.com
Dalili ya tatu; wateja wako hawana furaha kama waliyokuwa nayo mwanzo.
Unapoanza biashara na ukaweka juhudi kubwa mwanzoni, wateja wanapata huduma nzuri na kufurahia sana. Kwa furaha hii huanza kuwaambia wengine na huendelea kufurahia kuwa sehemu ya biashara yako. sasa inapofika wakati hali hii ikaanza kushika na hatimaye kutoweka kabisa, jua mabadiliko yanahitajika kwa sababu kuna kitu ambacho hakipo sawa.
Unapoona hamasa ya wateja inashuka, jua kuna kitu ulikuwa unafanya mwanzo na sasa hufanyi au kuna vitu walitegemea na sasa hawapati. Fanya tathmini ya biashara yako ili uweze kurudisha hamasa hii ya wateja wako.
Kuna dalili nyingi ambazo unaweza kupimia maendeleo ya biashara yako, hizi tatu ni muhimu sana na unapoona yoyote kati ya hisi kaa chini na itathmini biashara yako na ufanye mabadiliko. Usipofanya hivi maana yake umekubali biashara yako ife huku wewe unaiangalia.
Kama unahitaji ushauri zaidi juu ya changamoto za biashara unazopitia piga simu 0713 666 445 na utapata ushauri wa kina.

Kama ulivyokuja hapa na kupata maarifa bure kabisa usiache kuja kila siku kuangalia mapya tuliyokuwekea. Ukijenga utamaduni wa kutembelea ukurasa huu kila siku ndani ya muda mfupi utabadilika sana na kupiga hatua katika mambo yako unayoyafanya. Karibu tena na tena na usiache kushea na mwenzio ukurasa huu nae apate maarifa. 

JIFUNZE BIASHARA, PENDA BIASHARA.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT