Siku chache baada ya mamlaka ya shirika la ndege Tanzania (ATCL)
kutangaza viwango vya nauli za ndege katika mikoa kadhaa nchini ikiwemo
Kigoma, kumeibuka mjadala mzito hasa kwa wananchi wa Kigoma ambapo
Kupitia ukurasa wake wa facebook Mbunge huyo wa Kigoma mjini aliandika
hivi...
"Nimepata malalamiko ya watu wa Kigoma
kuhusu nauli Mpya za ndege za ATCL. Kwanza, ni dhahiri kwamba nauli
zilizotangazwa zimepunguza gharama za usafiri wa Anga Kwa zaidi ya nusu (
kuna Shirika moja tulikuwa tunalipa tshs 1.4m kwenda Na kurudi ilhali
ATCL imetangazwa itakuwa tshs 610,000 ). Hata Hivyo, Hata wataalamu wa
usafiri wa Anga wanasema tofauti ya nauli kati ya Mwanza Na Kigoma Ni
kubwa mno ukilinganisha Na umbali kuelekea huko kutokea Dar Es salaam.
Baada ya utafiti wa
kina, nimejiridhisha kuwa ATCL wanatulangua wasafiri wa Kigoma.
Nimewasilisha malalamiko rasmi kwenye mamlaka husika ili yafanyiwe Kazi.
Siku za usoni itabidi Nchi iwe Na
mamlaka ya kudhibiti bei katika usafiri wa Anga Kama ilivyo Kwa SUMATRA
kwenye usafiri wa majini Na Nchi Kavu. Mamlaka ya Usafiri wa Anga ( TCAA
) inaweza kupewa jukumu hili Pia. Hii itasaidia malalamiko
kushughulikiwa kisheria za Biashara badala ya kisiasa Kama ilivyo Sasa.
Natumai kuwa Watanzania wanaosafiri
kwenda Na kutoka Kigoma Kwa ndege wataweza kupata unafuu wa bei bila
kuathiri biashara ya Shirika la ndege la ATCL".
Kwamujibu wa shirika la ndege Tanzania (ATCL), Nauli halisi zitakuwa kama ifuatavyo;-
- Dar es Salaam – Mwanza kwenda ni shilingi 160,000 hivyo kwenda na kurudi ni shilingi 320,000.
- Dar es Salaam – Kigoma kwenda ni shilingi 395,000 hivyo kwenda na kurudi ni shilingi 610,000.
- Dar es Salaam – Arusha kwenda ni shilingi 180,000 hivyo kwenda na kurudi 360,000.
- Arusha – Zanzibar kwenda ni shilingi 249,000.
- Zanzibar – Dar es Salaam ni shilingi 123, 000.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT