Pablo de Greiff, Christof Heyns na Maya Sahli-Fadel walitoa ripoti yao kuhusu Burundi mwezi Septemba
Burundi imewapiga marufuku wachunguzi watatu wa Umoja wa Mataifa
baada yao kuchapisha ripoti wakiituhumu serikali kwa kutekeleza ukiukaji
mkubwa wa haki za kibinadamu.
Wachunguzi hao, kwenye ripoti mwezi jana, walisema maelfu ya watu
waliteswa, wakanyanyaswa kingono au wakatoweka wakati wa machafuko ya
kisiasa yaliyotokea tangu Aprili mwaka jana.
Aidha, walitahadharisha kuhusu uwezekano wa kutokea mauaji ya halaiki kutokana na kuongezeka kwa machafuko.
Uamuzi huo wa Burundi umetokea siku chache baada ya taifa hilo kutangaza
kuwa litajiondoa kutoka Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita
(ICC).
Barua iliyotiwa saini na waziri wa mambo ya nje wa Burundi Alain Aime
Nyamitwe ilisema Pablo de Greiff anayetoka Colombia, Christof Heyns
kutoka Afrika Kusini na Maya Sahli-Fadel wa Algeria hawatakikani tena
Burundi.
Ripoti waliyokuwa wamechapisha walisema kuna "ushahidi mwingi wa
ukiukaji mkubwa wa haki za kibinadamu" ambao kuna uwezekano ukawa ni
uhalifu dhidi ya binadamu, na ambao umetekelezwa na serikali ya Burundi
na watu wanaoiunga mkono.
Maandamano yamefanyika Bujumbura kupinga ripoti hiyo ya Umoja wa Mataifa
Tangazo kwamba Burundi itajiondoa kutoka mahakama ya ICC lilitolewa wiki iliyopita miezi sita baada ya mahakama hiyo yenye makao yake makuu mjini The Hague, Uholanzi kusema ingechunguza ghasia zinazoendelea nchini humo.
Umoja wa Afrika (AU) mara kwa mara umeituhumu mahakama hiyo kwa kuwabagua Waafrika.
Burundi yakataa polisi wa UN
Ghasia zilianza Burundi Aprili 2015 baada ya Rais Pierre Nkurunzinza kutangaza angewania urais kwa muhula wa tatu.
Tangu wakati huo zaidi ya watu 500 wamefariki na wengine 270,000 kukimbilia nchi jirani.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT