Zijue Sababu Kwanini Hutaki Kubadilika. | Bepari Classic
Breaking News
Loading...

Jumatano, 15 Februari 2017

Zijue Sababu Kwanini Hutaki Kubadilika.

Habari nyingine tena mpenzi msomaji wetu wa blogu yetu. Ni yangu matumaini u mzima wa afya. Hongera kwa siku nyingine tena. Kila siku kataka maisha yetu ni bora. Endelea kutumia vyema siku hii tena ili uzidi kuwa bora kuliko jana.

Mpendwa leo nitakuletea sababu nne za kwanini hutaki kubadilika kutoka mazoea/tabia hasi kwenda kwenye tabia chanya. Ni muhimu ukawa unafahamu ya kuwa bila kufanya mabadiliko makubwa ya kitabia na/au mazoea ni ngumu kufika katika lengo kuu la maisha yako. Mimi mwenyewe nilipoaanza tu safari yangu ya kuhakikisha natimiza ndoto zangu, cha kwanza nilianza kushughulika na tabia zote ambazo zilikuwa kikwazo kwangu. Leo katika mada hii nitalenga hasa kukuonesha hizi sababu ili ujue nini kina kukwamisha. Kujua sababu hizi itakuweka katika nafasi nzuri ya kuanza kushughulikia na sababu hizo.

Zifuatazo ni sababu zinazokusabisha usibadilike na kuwa na tabia chanya:-
Moja, Kutokuwa na Shauku la Mabadiliko.
Mabadiliko ni ngumu kutokea kwa mtu yeyote kama atakosa shauku au haja ya kubadilika. Shauku ni hali muhimu sana katika safari hii ya mabadiliko. Na shauku hujengwa na wewe mwenyewe baada ya kutamani mabadiliko na ukafika wakati mwenyewe kutoka ndani unaona haja kubwa ya kubadilika. Ni bahati mbaya kama hujafika hatua hii utajikuta kila mara unajaribu mabadiliko yako ya mazoea lakini baada ya muda kidogo unachemka.
Mimi nilifika hatua yakuamua kubadilika baada ya kukataa maisha niliyokuwa nayaishi awali. Niliona ni maisha ya shida na taabu kubwa, yalikuwa ni maisha ya fedhea. Kwa sababu ilifika mahali hata akiba ndani huna. Au mara nyingine huna hata fedha kidogo ya kukuwezesha kuwafanya wakupendao kufurahi. Yote hayo na mengine mengi yalichangia kuamsha shauku kubwa ndani yako ya kutaka mabadiliko makubwa. Kadhalika usomaji wa vitabu vya kuhamasisha na vitabu vya watu waliofanikiwa, umechangia pakubwa sana kuamsha shauku kubwa ndani yangu.
Pili, Kutokuwa na Nidhamu ya Mabadiliko. Kutokuwa na nidhamu ya mabadiliko ni kitu kingine ambacho hukwamisha kabisa safari ya mtu ya mabadiliko ya mazoea. Ndiyo maana katika makala zangu nyingi nimekuwa nasema sana kuhusu nidhamu katika kila jambo. Nidhamu ni ile hali ya utii wa kutekeleza ulioagizwa, au uliyojipangia au kutekeleza wajibu wako kulingana na taratibu zilizopo.
Nidhamu ni moja ya tabia muhimu sana katika safari yako ya kusaka mafanikio. Kama huna tabia hii, tafadhali chukua hatua kuijenga. Ndiyo, anza kujijengea hii tabia. Uliweza kujijengea tabia mbovu hadi leo zinakusumbua inakuwaje iwe ngumu kujijengea tabia nzuri. Kitu ambacho ni vyema kukijua ni kwamba kiasili  binadamu hupinga mabadiliko yoyote. Hivyo unapoanza mabadiliko uwe unalijua hili kwamba utapata ukinzania kutoka hata kwako mwenyewe, lakini kadri utakavyopingana na mwili ndivyo utakavyofanikiwa kujijengea tabia mpya.
Tatu, Kukosa Imani Kwamba Unaweza Kubadilika. Ukikosa imani kwamba unawezi badilika ni ngumu kufanya mabadiliko. Kumbuka imani huja kwa kusikia na kusikia huja kwa kusoma, leo jenga imani hii “ninaweza kubadilika na kuachana na tabia zote hasi” ninakwambia hivyo sina maana ya kutaka kukudanganya au kukuvutia, la hasha. Leo hapa unasoma makala hii kutoka kwa mtu ambaye aliamua kufanya mabadiliko makubwa katika maisha yake, unataka kumjua mtu huyo? Bila shaka ni mimi hapa.
Hakuna tabia ambayo huwezi kuiacha, hizo ni hofu tu ndogo ndogo, zilinitesa hata mimi lakini sikurudi nyuma. Nilikazana mpaka sasa nafurahia mabadiliko hayo, na ninazidi kupambana kubadilika zaidi. Kubadilika ni mchakato, unaanza taratibu kufanya tofauti ulivyozoea na hatimaye unabadilika kabisa. Ili ufanikishe hili anza leo kwenda kinyume na mazoea yako. Utashanga, maana utaanza kuona kumbe inawezekana.
Nne, Kutokujua Umuhimu wa Mabadiliko. 
Kutokujua umuhimu wa kubadilika ni moja ya sababu inayokufanya upambane na mabadiliko. Ubongo wako usipoona sababu za msingi ni ngumu kuweza kuachilia nguvu ya kuyahitaji au kuyatunza mabadiliko. Wengi hawabadiliki kwa sababu hawaoni umuhimu wake kabisa. Hawaoni nini tofauti ya kubadilika au kutokubadilika.
Kitu bora ni kwamba kabla ya kuchukua hatua ni vyema ukaorodhesha sababu zako za kwanini ubadilike. Hii itakusaidia kuifanya akili yako kuwajibika juu ya mabadiliko uyatakayo. Na baada ya kuzihorodhesha sababu hizo anza kuwa unazipitia kila mara. Ni muhimu sana kujua sababu, na mara nyingine hili liambatane na ujenzi wa picha kubwa kichwani, pichaya wapi unakotaka kufika. Picha hiyo kubwa itakujengea hamu kubwa ya kutamani kufikia mabadiliko yako.
Asante kwa kuwa nami, endelea kuwa kuwa nasi kwa makala zaidi. Tunakutakia safari njema ya mafanikio. Kwa mawasiliano yoyote tumia anuwani ya barua pepe hapo chini.
Ni mimi mwalimu wako,
Bepari. 

SOMA: IMANI ZINAZOKUZUIA USITAJIRIKE

 Ukijenga utamaduni wa kutembelea mtandao huu kila siku muda si mrefu unakuwa tajiri wa mali, maarifa na afya. Kazi kwako!
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT