USHAURI; Hatua Tano Za Kuchukua Kwa Mwalimu Anayetafuta Ajira Lakini Hajapata. | Bepari Classic
Breaking News
Loading...

Alhamisi, 10 Novemba 2016

USHAURI; Hatua Tano Za Kuchukua Kwa Mwalimu Anayetafuta Ajira Lakini Hajapata.

Habari ndugu yangu mwana mafanikio mwenzangu? Upendo nilio nao kwako si wa kawaida, nimetenga muda wangu leo kukushauri kijana mwenzangu ambae umemaliza masomo yako kwa ngazi ya astashahada, stashahada au shahada ya masomo ya ualimu na kwa sasa upo ukisubiria ajira kutoka serikalini.

Je wewe ni mwalimu? Je umekuwa unatafuta kazi bila ya mafanikio yoyote? Leo nataka nikushirikishe mambo matano unayoweza kuanza kuyafanya mara moja na ukaondoka kwenye hali ya kutokuwa na ajira uliyopo sasa.
teaching materials

Sasa mimi sitaki nikuchoshe na mengi hapa, nataka uniambie kama kweli una njaa na hasira ya kutoka hapo ulipo sasa, kwa kufanya lolote ambalo utahitajika kufanya.
Na kama ni ndiyo basi hapa nakushauri mambo matano (5) ya kuanza kufanya kesho....
1. Andika barua ya kuomba nafasi ya kufundisha kwa kujitolea bila ya kulipwa chochote, na chagua shule kumi zilizopo kwenye eneo linalokuzunguka, shule za sekondari au za primary kwa english medium. Katika shule kumi, hutakosa hata mbili ambazo watakuita kuongea na wewe, waombe wakupe nafasi ya kujitolea kufundisha, wakikupa nafasi hiyo, fanya kazi iliyo bora mno, wafundishe watoto vizuri mno, kiasi kwamba thamani yako iongezeke, fursa zaidi zitakuja.
2. Kwenye eneo unalokaa, ongea na wazazi wote ambao watoto wao wanasoma sekondari au hata primary, kisha waombe uwafundishe kwa muda wa ziada, jioni au mwisho wa wiki. Tafuta eneo unaloweza kufanyia zoezi hilo, waombe uanze kufundisha hata bure kwanza, halafu wakiona mabadiliko kwa watoto wao, ndiyo uanze kuwachaji kidogo. 

3. Kwenye eneo unalokaa, kama kuna watu wenye uwezo kiasi ambao wana watoto wanaosoma, unaweza kuongea nao na ukawa unawafundisha watoto wao majumbani kwao. Popote unapopata nafasi fanya kazi bora sana.
http://beparilakihaya.blogspot.comhttp://beparilakihaya.blogspot.com
 
4. Anzisha blog, ambayo inawafundisha wageni kiswahili fasaha, wewe ni mwalimu wa kiswahili, hivyo tengeneza mfumo ambao unaweza kumsaidia mtu asiyejua kiswahili akajifunza vizuri, mwanzo hutakuwa na wasomaji wengi, ila wewe target wale ambao ni wageni, na wapo wengi mno, kuna wachina wana njaa ya kukijua kiswahili.
Nyongeza, hapo kwenye blog toa huduma ya translation, labda kingereza kuja kiswahili, au kama unaweza kiswahili kwenda kiingereza. Kuna wengi wanahitaji huduma hiyo.
5. Kaa chini na wazo lolote la biashara ambalo unalo kwa sasa, ambalo upo tayari kutoa kila tone la jasho lako kufanyia kazi, yaani iwe passion yako kweli. Liandike wazo hilo vizuri, angalia ni sehemu ipi ya chini kabisa unayoweza kuanzia, kiasi kidogo kabisa unachoweza kuanza nacho. Kisha waangalie watu wote wanaokuzunguka, ambao una mahusiano nao ya kindugu au kirafiki. Wachague wale ambao unajua watakuelewa, kisha zungumza nao kwa namna wanavyoweza kukusaidia kwa wazo hilo ulilonalo.
Anza na hayo, unaweza kuchagua mawili au matatu au yote na uone lipi litawezekana kwako, ila blog anza nayo hata kesho, miaka mingi ijayo utajishukuru sana.
Kama kwa namna yoyote ile wakati unasoma huo mtiririko napo ulikuwa unajiambia mimi siwezi hili au siwezi hili, niseme tu hutaweza kutoka hapo ulipo.
Nimalize kwa kukuambia kwamba kama umechagua kitu cha kufanya hapo, na ukishajipanga kufanya, nitafute, nitakucoach bure kabisa, ukishakuwa na mpango tayari. 
Nakutakia utekelezaji mwema wa yale ambayo umejifunza,

Kama kawaida yetu wanamafanikio huwa hatupendi kutoka peke yetu, nakuomba uwashirikishwe wenzako ushauri huu kwa kushea ukurasa huu nao waweze kupata ulichokipata.  Ubarikiwe.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT