MBINU MUHIMU ZA KUJENGA MAFANIKIO KATIKA BIASHARA . | Bepari Classic
Breaking News
Loading...

Jumatano, 30 Novemba 2016

MBINU MUHIMU ZA KUJENGA MAFANIKIO KATIKA BIASHARA .

Image result for BIASHARAWajasiliali wana mchango mkubwa katika  maendeleo ya uchumi wa nchi yetu.
Chimbuko la vipato ambavyo husaidia kuvunja mzunguko wa umasikini  hutoka kwa wajasiliamali  kupitia biashara zao. Ujasiriamali ni mkombozi wa wengi!

Kuna mbinu mbalimbali  ambazo wajasiriamali wanaweza kuzitumia ili kujenga mafanikio katika biashara zao.
1. Fanya kile unachokipenda .
Kama wewe ni mjasiriamali ni muhimu kufanya biashara ya kile kitu unachokipenda usiingie tu katika biashara kwa kufanya kile ambacho umeona tu wengine wanafanya usifanye kwa kuiga au kufuata mkumbo.
  • Ikiwa  wewe umefanya  kazi kwa mda mrefu katika hotel  na una kiu kubwa ya kuwa mjasiriamali, ni vema ukafikiria ni kitu gani katika tasnia hiyo ya hoteli unaweza ukaifanya wewe mwenyewe binafsi vizuri zaidi.
Kwa mfano, ikiwa katika tasnia hiyo ya hoteli umefanya kazi kama mpishi  kwa mda mrefu au muandaaji wa  mikutano, kwa nini usifikirie kuanzisha kitu chako ambacho una uzoefu nacho mzuri zaidi na kuona  kwa namna gani Siku za baadae utaweza kujitegemea. ikiwa wewe ni mjasiriamali wa mda mrefu basi inakupasa kujenga hari ya kupenda hicho ambacho unakifanya.
✍baadhi ya wajasiriamali wamevunjika moyo kwa kuona  hawapati matokeo mazuri kwa Yale wanayofanya  labdawangependa "watoke'' haraka


Kumbuka ndugu mjasiriamali mafanikio katika biashara si suala la kulala na kuamka Bali ni kitu kinachoweza kuchukua mda na huhitaji uvumilivu. jifunze Toka kwa wajasiriamali waliofanikiwa na utagundua kwamba mafanikio yao yalichukua mda mrefu. 

2. Jenga upekee  wa kile unachofanya. ili kupata mafanikio unahitaji kujenga upekee katika kile  unachofanya. .
jaribu kuwa mbunifu kwa kile ulichoamua kufanya tafta  namna ya kujitofautisha na washindani wako, ufahamike kwa namna yako.wajasiriamali wengi wamefanya mambo kwa kuona tu wengine wanafanya.
 Wengi wameigia katika biashara kwa kuiga toka kwa wenzao Yale wanayofanya. Yafaa mjasiriamali kuwa mbunifu na kuacha kuiga kila unachokiona kutoka kwa wenzako.ni muhimu kwa wajasiriamali kuwa na upekee wa bidhaa au huduma kwani ni njia nzuri ya kudhibiti soko
elewa  biashara katika zama hizi zina ushindani mkubwa na changamoto ni nyingi. sasa ili kukabiliana na changamoto hizo inapaswa kujitofautisha.

3. Jiulize unafanya nini kuwashika wateja wako ?
wateja ni msingi wa kuendelea kwa biashara yoyote kwa sababu bila wateja wa kuwauzia bidhaa  akuna biashara itakayoendelea. wateja ndio wanaofanya shughuli zote unazozijua ziendelee.
✍jijengee utamaduni Kama mjasiriamali  wa kuwashika wateja wako, hili unaweza kulifanya kwa kujenga uhusiano mzuri na wateja wako.hakikisha wateja wanapata mile wanachoitaji na epuka kuwa sehemu ya maudhi kwa wateja lugha nzuri inalipa!
☺️jiulize katika biashara yako umewai kufanya nini katika kuwathamini wateja wako. Kama  wateja  wanaona unawajali na kuwathamini basi nao pia watakujali kwa kuendelea kufanya biashara na wewe kwa mda mrefu na watazidi kukuamin. Zaidi ya kuendelea kuwa na wewe wateja walioridhika na wewe  watakuw chanzo kizuri cha kutangaza biashara yako kwa wengine.

4.Jenga mtandao.
Pamoja na kuwa  na namna bora ya kuwashika wateja wako ni muhimu kujenga mtandao mzuri na wengine  (network). kuwa mtu wa kujichanganya  na wengine "usijifungie vioo" usione washindani wako kama maadui
  • Ninapozungumzia kujenga mtandao maana take ninkutafuta namna bora ambayo itakufanya wewe na biashara yako mfahamike bila gharama kubwa.
Zaidi ya ili ni muhimu kujiunga na taasisi mbalimbali za kibiashara ili kuweza kupata fursa .
Kuna maonyesho mbalimbali ya kibiashara  yanayofanyika hapa nchini na nje ya nchi Ila huwa ni fursa kwa wenye kufahamu ❕amka mjasiriamali usiweke usiku

Ukijenga utamaduni wa kutembelea mtandao huu kila siku muda si mrefu unakuwa tajiri wa mali, maarifa na afya. Kazi kwako!

Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT