Mhe. Waziri ametoa agizo hilo leo alipozungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Mjini Dodoma katika mkutano na vyombo vya habari ambapo aliwataka Wakuu wa Mikoa kusimamia zoezi hili kikamilifu na kuhakikisha madawati yaliyotengenezwa yameingizwa kwenye vyumba vya madarasa na sio kutoa taarifa ya kuwapo kwa madawati hayo kwa mafundi.
“ Wakuu wa Mikoa wanatakiwa kuja na taarifa sahihi ya idadi ya madawati iliyopo ukilinganisha na mahitaji vinginevyo tutadanganyana kwamba madawati yapo mengi lakini kumbe baadhi ya watoto wanakaa chini” alisisitiza Mhe. Simbachawene
Alisema kuwa kuna baadhi ya Mikoa wana madawati mengi lakini hayajafika kwenye shule zenye upungufu hivyo ni jukumu la wakuu wa mikoa kuhakikisha kuwa madawati hayo yanafika mashuleni kwa wakati.
Mhe. Waziri alisema kuanzia Disemba 2015 Serikali ilianza kutekeleza sera ya Elimu Msingi bila malipo na kutokana na utekelezaji huo,mwitikio wa wananchi kupeleka watoto shuleni umekuwa mkubwa na kuleta changamoto ya upungufu wa miundombinu muhimu kama vile vyumba vya wadarasa na matundu ya vyoo.
Aidha, Mhe. Simbachawene ametoa rai kwa wazazi,walezi na jamii kwa ujumla kutochoka kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuboresha miundombinu hiyo muhimu kwenye shule kama walivyotoa ushirikiano wa dhati kukabiliana na upungufu wa madarasa.
Mnamo tarehe 16 Machi, 2016, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. John Pombe Mgaufuli aliagiza kuwa kusiwepo na mtoto anayekaa chini kwa kukosa dawati. Halmashauri kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa Elimu nchini wametekeleza agizo hilo kwa kiwango kikubwa.
Kabla ya agizo hilo mahitaji ya madawati kwa shule za Msingi yalikuwa 3,252,313 na katika shule za Sekondari 1,495,610. Hadi sasa madawati yaliyopo ni 3,319,355 kwa shule ya Msingi na kufanya kuwa na ziada ya madawati 66,042 na kwa upande wa Sekondari madawati yaliyopo ni 1,540,625 na kufanya kuwa na ziada ya madawati 45,015.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT