Mtangazaji mahiri wa kipindi cha Amplifaya cha Clouds FM, Millard Ayo
wakati akitoa salamu zake za rambirambi kufuatia vifo vya wanafunzi 32,
walimu 2 pamoja na dereva mmoja, amefunguka kuzungumzia namna
alivyonusurika kwenye ajali kama hiyo akiwa mdogo.
Katika ajili hiyo ambayo amedai ilitokea mwaka 1994 mkoni Arusha
Ngorongoro, ilisababisha vifo vya wanafunzi wenzake wanne ambao alikuwa
nao kwenye safari hiyo ya kuelekea Serengeti.
Akiongea Jumatatu hii, Millard Ayo amedai katika ajali hiyo alimpoteza rafiki yake ambaye alikaa naye siti moja.
“Pole sana kwa familia za Arusha najua ni kiasi gani sasa hivi watu wana
huzuni sana, watu 32 kwa wakati mmoja ni kitu kikubwa sana,” alisema
Millard.
“Na mimi hii ajali nilipoisikia tu ni wanafunzi imenikumbusha mbali sana
kwa sababu hata mimi mwenyewe niliwahi kupata ajali kama hiyo mwaka
1994 tulikuwa Ngorongoro sehemu moja maarufu inaitwa Malanja Cross.
Tulikuwa na gari la jeshi wanafunzi wa shule ya msingi, Patandi Primary
Schools Tengeru Arusha tukielekea Serengeti kuangalia wanyama lakini
bahati mbaya gari ikafeli breki ikaingia bonde la ufa, wakafa wanafunzi
wenzangu wanne akiwemo rafiki yangu ambaye nilikaa naye siti moja,”
aliongeza Millard.
Mtangazaji huyo amedai yeye wakati basi hilo likibiringika, alikuwa
amebanwa na chuma kichwani hivyo hakuweza kutoka mpaka watu walivyokuja
kumwokoa.
Pia amesema aliumia vibaya katika mguu wake wa kushoto.
Credit - Bongo 5
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT