Mzee Kikwete hupenda kusema, ‘’akili za kuambiwa, changanya na zako’’.
Maalim Seif na wapambe wake wa Zanzibar walikubali akili za kuambiwa lakini hawakuchanganya naza kwao.
Maalim Seif hakufahamu kuwa washauri wake wakubwa ni CCM B ambao
hawakumtakia mema na kama alifahamu basi alitakiwa achukue ushauri wao
na kuchanganya na akili zake.
Kama angechanganya na akili zake kwa sasa CUF isingekuwa katika hali
iliyopo kwa sasa. CUF ya kabla ya Uchaguzi Mkuu 2015 sio hii ya leo
ambayo inagawana vito kila siku.
Kwa sasa amezunguka dunia nzima akipiga kelele kuhusu kuibiwa kura huku
akiwaaminisha wapambe wake yuko mbioni kuingia Ikulu ya Zanzibar kabla
ya 2020 lakini ukweli unazidi kumsuta kila siku.
Baada ya kuzunguka dunia nzima kwa sasa amehamia mpaka kwa wachungaji
kama Josephat Gwajima kama mentor wake. Hii ni dalili inayoonyesha
desperation and kicking a dead horse.
This is an enormous leap for Maalim Seif, catapulting him to a new level of obscurity.
Kinachofanywa kwa sasa na UN, EU wakisaidiwa na Marekani kinatoa
maandiko ukutani kuwaambia wale ambao wanadhani Maalim Seif ataingia
Ikulu ya Zanzibar kabla ya Uchaguzi Mkuu 2020 wasipoteze muda wao.
Ieleweke kuwa fimbo ya kuichapia serikali ya Mapinduzi Zanzibar ilikuwa
ni kuinyima misaada au kuweka shinikizo kubwa kwa serikali ya Tanzania.
Kinachofanyika kwa sasa ni kinyume chake kwa maana nyingine, Wazungu
wanamwambia Maalim Seif, Let bygones be bygones.
Ninatumaini Uchaguzi Mkuu ujao, Maalim Seif atachangaza na akili zake baada ya kura kuanza kuhesabiwa.
Hii sio dalili nzuri kwa Maalim Seif na CUF Zanzibar.
Waingereza husema, ‘’Sometimes you’ll never know the value of what you have until it’s gone’’.
Nimalize kwa kusema, A Chinese military general, strategist and
philosopher, Sun Tzu once said, If you know the enemy and know yourself,
you need not fear the result of a hundred battles. If you know yourself
but not the enemy, for every victory gained you will also suffer a
defeat. If you know neither the enemy nor yourself, you will succumb in
every battle.
Source - Jf
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT