
Kupitia kipindi cha TakeOne kinachorushwa na CloudsTv Saida Karoli
anasema yeye alikuwa haelewi masuala ya mikataba. Hivyo alijikuta
mikataba ilionyesha kwamba haki za malipo ya nyimbo zake zilikuwa kwa
meneja wake. Mfano, alipofuatilia malipo baada ya Diamondplatnumz na
Rayvanny kurudia wimbo wake #Salome, alikuta kwamba aliyekuwa meneja
wake ameshalipwa na yeye akaja kuambulia pesa kidogo tu ( ' pesa ya soda
' )
Lakini SaidaKaroli anasema yeye wimbo huo ni kama aliutoa bure kwa
Diamondplatnumz na anamshukuru sana kwani kitendo cha Diamond kurudia
wimbo huo kimekuwa na faida kwake.

"Hata ningekuwa na haki ya kushtaki, nisingemshtaki @diamondplatnumz.
Mimi ni kama nilikuwa nimekufa na aliporudia huo wimbo nimefufuka. Hivyo
kwa moyo mmoja......nisingeweza kumshatki na ninamshukuru." -
#SaidaKaroli. .
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT