
Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista Wasabato mkoani Mara, George
Ojwang’ amewaagiza wachungaji na wazee wa kanisa hilo kuwashughulikia
waumini wao wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya.
Aliyasema hayo katika sherehe za kumsimika mchungaji mpya wa Mtaa wa
Mauwe ulioko Kitembe Rorya. Alisema kama kanisa litakuwa safi, Serikali
haitakuwa na muda wa kushughulikia watu kama hao wanaosababisha kupotea
kwa nguvu kazi ya Taifa.
Katika tukio jingine, Mkoa wa Tabora umezindua kampeni ya kupambana na
dawa za kulevya na wahusika wakionywa kutofanya mzaha katika vita hiyo.
Akizungumza kwenye uzinduzi wa kampeni hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita
mjini hapa, Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri alisema tayari kamati
zote za ulinzi na usalama za wilaya zimepewa maelekezo ya kufanya.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Hamis Issa alisema kati ya Februari 13
na 16 wamekamata dawa za kulevya mbalimbali zikiwamo cocaine, mirungi,
bangi na mbegu zake.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT