Mbunge wa zamani Kinondoni, Iddi Azzan amezungumzia sakata lake na Jeshi
la Polisi baada ya kukaa mahabusu kwa siku mbili alikokuwa akihojiwa
kuhusu kuhusishwa kwake na masuala ya dawa za kulevya.
Mapema jana akiwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam, Azzan
alisema aliingia katika orodha ya watuhumiwa kwa kuwa amekuwa akisemwa
katika mitandao ya kijamii kwa muda mrefu.
Hata hivyo, alisema alifurahishwa na kitendo cha kutajwa kwenye orodha
ya wanaojihusisha na biashara hiyo akiamini kwamba hatimaye suala hilo
litafikia mwisho.
“Bora nilivyotajwa huenda suala hili litaisha kwa kuwa nimeanza kusemwa
tangu mwaka 2011. Cha ajabu ni kwamba awali nilituhumiwa kujihusisha na
biashara sasa hivi napimwa kuona kama natumia.
Mbunge huyo pamoja na Askofu Josephat Gwajima walitoka polisi saa 10:28
baada ya kuitukia wito uliowataka kuripoti hapo jana saa nane mchana.
Wakati Azzan aliondoka kituoni hapo kwa gari aina ya Toyota Rav 4 ‘short chassis’, Askofu Gwajima aliondoka kwa teksi.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT