Kanye West ana mabadiliko ya hisia zake za moyoni. Unakumbuka aliwahi
kusema kuwa kama angepiga kura angemchagua Donald Trump? Alienda mbali
zaidi na kukutana na Rais huyo New York.
Na sasa Yeezy amerudisha kadi yake, hamuungi tena mkono. Kwa mujibu wa
TMZ, Kanye ameziondoa tweets zote alizoandika kumfagilia Trump.
Mtandao huo umesema rapper huyo amechukizwa na sera za kibaguzi za rais huyo wa 45 ikiwemo ya kuwazuia waislamu kuingia Marekani.
Kanye alikuwa mmoja wa wasanii wakubwa wachache waliokuwa upande wa Trump. Hata mkewe Kim Kardashian, ni mmoja wa mastaa wanaompinga vikali rais huyo.
Mwezi uliopita rapper T.I. alimuita Kanye msaliti.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT