Hiki ndicho Alikiba alichowaambia Sony Music kuhusu mashabiki wake | Bepari Classic
Breaking News
Loading...

Jumamosi, 18 Februari 2017

Hiki ndicho Alikiba alichowaambia Sony Music kuhusu mashabiki wake

 Alikiba akiteta jambo na CEO wa Sony Music Africa, Sean Watson

Alikiba ameyasikia malalamiko ya mashabiki wake kuhusu ukimya wake wa hapa na pale na amekiri huumia sana kuona wakimrushia lawama.
Kutokana na ukweli huo, hitmaker huyo wa Aje amedai kuwa amelazimika kuwaambia mabosi wa Sony kuwa wajipange vyema ili kuhakikisha kuwa mashabiki wake wanaridhika.
Kwenye interview na millardayo.com, Alikiba amedai kuwa CEO wa Sony Music Africa, Sean Watson, ameiambia bodi ya label hiyo jinsi Alikiba alivyo na mashabiki wengi nyuma ambao panapotokea kuchelewa kwa lolote, ‘hung’ata kama nyuki.’
“Kwahivyo they have to make sure kila kitu kinaenda on point, kila kitu hakitakiwi kudelay, kila kitu kinakwenda sawa,” amesema Kiba.
“Yaani they have to make sure kwamba hawadisappoint fans wangu, kwasababu pressure ambayo wanapata yaani tayari Sean ameelewa kwahiyo wamekubali wamesema sawa, nadhani fans kitu hicho sasa nimekiacha mikononi mwa jamaa na kama kutakuwa na chochote mtakuwa mnapeleka malalamiko yenu kwao,” amesisitiza.

Kiba yupo nchini Afrika Kusini kwaajili ya ziara yake kubwa.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT