
Eric Omondi anapojitayarisha kuja na LIVE TV show yake ya comedy nchini
Tanzania, tayari moyo wake ulilowekwa na kulowa chepechepe na upendo
aliopewa na bado anaupata kutoka kwa mashabiki wa Bongo.
Ni baada ya kukutayarishia segments za comedy kama vile ”How to be like
Diamond” ambayo iliwachangamsha mashabiki wa Diamond kote Afrika kwa
kuiga vipengele fulani kwenye maisha binafsi ya staa Platnumz. Na
nyingine ”How to be like Magufuli” ambayo aliiga nakuelezea hulka za
Mheshimiwa rais wa sasa wa Tanzania Dkt John Magufuli, vipande hivi vya
video fupi za comedy kutoka kwa Eric Omondi unaweza vipata kwenye
channel yake ya YouTube.
Omondi ambaye kwa ajili ya Valantine ama siku ya wapendanao, alituletea
segment mpya kwa jina Adam and Eve, inayotamba na tayari ndani ya siku
sita zilizopita imefikisha zaidi ya views 144k, kwenye channel yake ya
YouTube, ametumia vipande vya muziki kutoka kundi la muziki la hapa
nchini Kenya la Heart The Band ”Nikikutazama” na kipande kidogo kutoka
kwa wimbo wa rapper mkali anayependwa kwa hivi sasa Darassa kwenye wimbo
wake ‘Muziki.’
Katika sehemu moja kwenye segment hii kutoka kwa Eric Omondi na mrembo
wake Chantal Graziola, ambaye pia ndiye mchumba wake Eric mwenye asili
ya kikenya na kitaliano, Chantal ambaye aliiga kama Eve, anaonekana
akimuamsha Eric (Adam) ili aule tunda alilopewa na nyoka kulingana na
vitabu vitakatifu. Na baada ya Eric kuamka, baadala ya kumpa tunda kama
wengi walivyotarajia Chantal Graziola anampa Eric ear-phone asikilize
favourite song yake, ambayo ni ngoma Muziki ya Darassa.
Darassa anakuwa staa wa pili kutoka Bongo baada ya Diamond kuugusa moya
wa Eric ambaye hajaweza kuficha hilo kwa kuamua kuutumia wimbo wake
Muziki…Pata uhondo zaidi kwenye kipande hiki cha comedy hapa chini upate
uhakikisho zaidi.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT