
Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo imesema haitoweza kumudu gharama za
uchaguzi wa Rais uliokuwa umepangwa kufanyika mwaka huu, serikali
imesema.
Waziri wa bajeti, Pierre Kangudia amesema gharama za kuendesha uchaguzi
ambazo ni dola bilioni 1.8 ni kubwa mno. Mwaka jana, serikali na
upinzani vilikubaliana kufanya uchaguzi mpya mwishoni mwa mwaka huu.
Utawala wa Rais Joseph Kabila ulimalizika November 2016. Wapinzani wa
Kabila wamemshutumu kwa kuendelea kuchelewesha uchaguzi ili aendelee
kukaa madarakani.
Kabila aliingia madarakani mwaka 2001 baada ya kuuawa baba yake, Laurent Kabila.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT