Zaidi ya kilo 400 za Samaki waliokuwa wakisafirishe kinyume na utaratibu zakamatwa Kagera. | Bepari Classic
Breaking News
Loading...

Jumanne, 13 Desemba 2016

Zaidi ya kilo 400 za Samaki waliokuwa wakisafirishe kinyume na utaratibu zakamatwa Kagera.

Kikosi cha ulinzi wa rasilimali za uvuvi  kanda ya Kagera kwa kushirikiana na jeshi la polisi kimefanikiwa kukamata sherena mzigo wa Samaki aina ya Sato na Sangara wenye uzito wa zaidi ya kilo 400 waliokuwa wamefichwa kwenye nyumba iliyoko katika kijiji cha Katanga kilichoko kata ya Magattakarutanga iliyoko wilayani Muleba, mkoani Kagera.

Samaki hao waliokuwa wamehifadhiwa kwenye majokofu makubwa matano na walikuwa wasafirishwe hadi jijini Dar es Salaam na mfanyabiashara aliyetajwa na afisa mfawidhi wa kikosi hicho Chacha Marwa kwa jina la Athumani kahauza ambaye amekimbia baada ya Samaki wake kukamatwa, akizungumza Marwa anaelezea kikosi chake kilivyofanikiwa kumnasa mfanyabiashara anayedaiwa kufanyabiashara ya kusafirisha samaki bila leseni.

Afisa huyo amezitaja sababu za kuwakamata na kuwataifisha Samaki hao kuwa ni pamoja kuvuliwa wakiwa wadogo, kuhifadhiwa katika mazingira hatarishi na mmiliki wa Samaki hao kufanya biashara ya kusafirisha bila leseni hivyo akawaonya wanaofanyabiashara ya Samaki bila kufuata utaratibu, kwa upande wake, Tilfrid Braison mmoja wa wafanyakazi wa mfanyabiashara huyo ameeleza kuwa kazi yao ni kuwapokea Samaki na kuwakata, naye mtendaji wa serikali ya kijiji cha Katanga Bagelize Bagwanga akieleza changamoto za kuuthibiti uvuvi haramu.  
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT