Mbuyu Twite akiitumikia klabu yake ya Yanga
Akithibitisha taarifa hizo, Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Baraka Deusdedith, amesema mkataba wa kiungo huyo ambaye mara nyingine hucheza kama mlinzi wa pembeni unamalizika mwezi huu, na tayari walikwishafanya naye mazungumzo kuwa hawata endelea naye.
Baraka amesema sababu kuu ya kumtema nyota huyo raia wa DRC ni kutokana na Yanga kumpata mbadala wake, ambaye ni Justine Zulu kutoka Zambia na kwamba kumuacha Mbuyu hakumaanishi kuwa hana kiwango, isipokuwa ni kupatikana kwa mbadala wake.
Mbuyu Twite baada ya kuwasili nchini Mwaka 2012 na kuvalishwa jezi
yenye namba sawa na jezi aliyokuwa ameandaliwa Simba na kutangazwa na
mwenyekiti wake enzi hizo, Ismail Rage
Ujio wa Mbuyu nchini Tanzania mwezi August mwaka 2012 ulitikisa anga la usajili katika vilabu vya Simba na Yanga kutokana na kuwaniwa na vilabu vyote viwili huku Simba wakidai kuwa walikwisha mlipa pesa za usajili, lakini akaangukia Jangwani na kukumbana na mapokezi ya aina yake katika uwanja wa ndege wa Dar es salaam.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT