Katika mwendelezo wake wa kuwapatia wateja wake na watanzania wote kwa ujumla burudani za sikukuu, Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na wasanii wa WCB imeandaa matamasha mawili ya kukata na shoka ambayo yatafanyika katika msimu huu wa sikukuu.
Mkuu
wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania,Nandi
Mwiyomella(kushoto)akimsikiliza Msanii wa muziki wa kizazi kipya wa
bongo fleva,Diamond Platinumz(kulia)akifafanua jambo kwa waandishi wa
habari(hawapo pichani)wakati wa hafla fupi ya kutanga tamasha la”Nogesha
Upendo”yatakayofanyika Disemba 24 katika fukwe za Jangwani Sea Breeze
jijini Dar es Salaam na Disemba 25 Iringa katika uwanja wa Samora chini
ya udhamini wa Vodacom Tanzania
Msanii
wa muziki wa kizazi kipya wa bongo fleva,Diamond
Platinumz(katikati)akipiga selfie na baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom
Tanzania mara baada ya mkutano na waandishi wa habari(hawapo
pichani)kuhusiana na tamasha la”Nogesha Upendo”litakalofanyika Disemba
24 katika fukwe za Jangwani Sea Breeze jijini Dar es Salaam na Disemba
25 Iringa katika uwanja wa Samora chini ya udhamini wa Vodacom Tanzania
Mwiyombella alisema burudani hii ya muziki inakwenda sambamba na promosheni ya Nogesha Upendo ya Vodacom inayolenga kuwapatia wateja wote wa mtandao wa Vodacom zawadi za sikukuu ikiwa ni shukrani kwa wateja ambapo pia wateja wanayo fursa ya kujishindia tiketi za bure za kushiriki katika matamasha haya makubwa katika msimu huu wa sikukuu.
Baadhi
ya wasanii wa nembo ya WCB wakiongozwa na Diamond Platinumz wakiwasili
katika makao makuu ya Vodacom Tanzania,yaliyopo Mlimani city jijini Dar
es Salaam katika mkutano na waandishi wa habari kuhusiana na tamasha
la”Nogesha Upendo”litakalofanyika Disemba 24 katika fukwe za Jangwani
Sea Breeze jijini Dar es Salaam na Disemba 25 Iringa katika uwanja wa
Samora chini ya udhamini wa Vodacom Tanzania
Naye Msanii wa muziki wa kizazi kipya anayetamba katika anga za kimataifa,Diamond Platinumz akiongea kwa niaba ya wasanii wa WCB alitoa wito kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam na Iringa kujitokeza kwa wingi siku ya shoo hizo kwani zitakuwa ni shoo za kihistoria katika mikoa hii miwili kufanywa na Vodacom kwa kushirikiana na WCB,Napenda kuwahakikishia mashabiki wetu kwamba tutakamua vilivyo tukiwa na wasanii wenzangu wote wa WBC kwa “Kunogesha Upendo,”alisisitiza Diamond.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT