Mwalimu akimuadhibu mwanafunzi
Baadhi ya wazazi wanafunzi katika shule za msingi na sekondari wilayani
Kilwa mkoani Lindi wameunga mkono adhabu ya viboko iendelee mashuleni
na kutoa wito wa sheria, kanuni na taratibu za utoaji wa adhabu hiyo
zifuatwe.
Wazazi hao wametoa kauli hiyo kwenye semina ya wadau wa elimu iliyoandaliwa na mtandao wa elimu Tanzania (TENMET) kwa kushirikiana na wadau wengine, kuhusu uwasilishaji wa matokeo ya utafiti wa mradi wa uhamasishaji wa elimu bora kwa kutumia rasilimali za ndani wilayani humo.
Wameongeza kuwa ili kudhibiti nidhamu ya wanafunzi shuleni itakayosababisha kupandisha kiwango cha ufaulu, kuna haja ya kuendelea kutumika, hata hivyo utekelezaji wake usitumike vibaya na kusababisha ukatili dhidi ya wanafunzi.
Aidha wazazi hao wamebainisha kuwa iwapo walimu watazingatia mambo hayo hakutakuwa na matukio mengi ya walimu kutenda vitendo vya kikatili dhidi ya wanafunzi.

Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT