Waziri mkuu ambaye yupo katika ziara ya kikazi mkoani Arusha ametoa agizo hilo mara baada ya kutembelea hospitali ya mkoa huo ya Mountmeru na kujionea msongamano wa wagonjwa katika wodi ya akina mama na watoto ambapo ameshuhudia wagonjwa watatu wakilala katika kitanda kimoja.
Amesema hali hiyo imekuwa ikihatarisha maisha ya wagonjwa lakini pia kuwapa kazi kubwa madaktari kuhudumia wagonjwa kutokana na msongamano huo.
Awali baadhi ya wagonjwa katika wodi ya wakina mama wameridhishwa na huduma zinazotolewa katika hospitali ya mountmeru lakini wakilalamikia huduma zinazotolewa katika hospitali ya Levolosi na ukosefu wa baadhi ya miundombinu kama vyoo katika hospitali ya Mountmeru.
Akikamilisha ziara yake hospitalini hapowaziri mkuu akamuagiza mganga mkuu wa hospitali ya Mountmeru Daktari Frida Mokiti kuchunguza tatizo linalosababisha wagonjwa kukimbia huduma zinazotolewa katika hospitali za levolosi,themi na ngarenaro na kuchukua hatua mara moja.
Ziara ya waziri mkuu kasim majaliwa katika hospitali ya mkoa wa arusha ya ,mountmeru imefuatia malalamiko ya mama mmoja ambaye aliibiwa motto katika hospitali hiyo miezi mitatu iliyopita ambapo hadi leo motto huyo hajapatikana.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT