Nchini
Mexico ambapo ulanguzi wa mihadarati umekithiri, wakuu wa magenge ya
ulanguzi wa dawa za kulevya huishi maisha ya kifahari na hutamani
kuendelea hivyo hata wanapokuwa wamekufa.
December
13 2016 BBC wameripoti kuwa nchini Mexico utakutana na makaburi ambayo
yangeweza kugeuzwa hata kuwa nyumba ambazo matajiri wengi wangejivunia
kuishi. Unaambiwa ni makaburi makubwa yaliyojengwa na kuwekwa huduma za
kisasa na vitu vingi vya anasa.
Kuna
baadhi ya makaburi yenye viyoyozi, kuna vioo visivyopenya risasi na
baadhi yana hata vyumba ambavyo wageni wanaofika kutoa heshima kwa wafu,
wanaweza kuketi na kupata kila kitu kinachopatikana katika nyumba za
kifahari.
Baadhi
yanakadiriwa kugharimu hadi Sh milioni 633 milioni, Makaburi mengi haya
hupatikana jimbo la Sinaloa, anapotokea mlanguzi mkuu Joaquin “El Chapo”
Guzman ambaye kwa sasa anazuiliwa na anatarajiwa kuhamishiwa Marekani
mwakani.
Katika
eneo moja la makaburi, Jardines del Humaya, katika mji mkuu wa jimbo la
Culiacan, ndipo unapopata baadhi ya makaburi ya kupendeza zaidi.
Kwa mujibu wa BBC kaburi moja ambalo
linadaiwa kuwa na mwili wa mlanguzi aliyetumiwa kuua watu, lina hata
kamera za kiusalama, pamoja na kioo kisichopenya risasi. Baadhi ya
makaburi yamejengwa kama nyumba za kisasa au makanisa madogo. Krismasi
inapokaribia baadhi huweka miti bandia ya Krismasi, lakini
kinachokosekana katika makaburi mengi ni utambulisho wa aliyezikwa
ndani.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT