Paul Makonda amesema zoezi la kusikiliza kero za wananchi litakuwa la kudumu | Bepari Classic
Breaking News
Loading...

Alhamisi, 1 Desemba 2016

Paul Makonda amesema zoezi la kusikiliza kero za wananchi litakuwa la kudumu

Mkuu wa Mkoa wa Dsm Paul Makonda amesema zoezi la kusikiliza kero za wananchi na kuzipatia Ufumbuzi wa papo kwa papo litakuwa la kudumu ili kumaliza migogoro na kero kutoka kwa wananchi na kuwataka watumishi katika idara zote za jiji la dsm na manispaa zake kujipanga ili kuzitatua kero zinazowakabili wananchi.

Akizungumza jana Usiku katika hafla iliyowajumuisha wakuu wa idara, taasisi zote za Umma za mkoa, wakuu wa polisi wa wilaya na kanda maalum iliyofanyika nyumbani kwake amesema nia yake si kumuonea mtu au kiongozi isipokuwa kurudisha nidhamu ya Uwajibikaji kwa wananchi.

Amewataka wenyeviti wa serikali za mitaa pamoja na watendaji kumaliza migogoro katika mitaa au kata zao kabla zoezi lingine la kutembelea kata kwa kata kuanza kwa kuwa viongozi watakaobainika kuhusika na migogoro hiyo hawatapona.

Baadhi ya Viongozi walizungumzia ziara hiyo ya kusikiliza kero za wananchi kuwa itasaidia kupunguza malalmiko lakini pia kutoa haki kwa wananchi wanyonge ambao wamekuwa wakidhulumiwa haki zao na wasijue wapi kwa kuzipata.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT