Akizungumza na waandishi wa habari mara bada ya kikao cha pamoja na viongzoi wa vyama vya siasa kuhusu maandalizi ya uchaguzi huo mkurugenzi wa tume hiyo ya uchaguzi nchini Kailima Ramadhan amesema tume haikukosea ila imefuata taratibu zote na kuvitaka vyma vya siasa kufahamu sheria za uchaguzi ambapo amesema endapo patatokozea chama kuibuka na wagombea wawili ni ishara kuwa kuna mgogoro na ndipo sheria hiyo inapotumika.
Mapema mwenyekiti wa Taifa wa tume hiyo jaji mstaafu Damian Lubuva amesisitiza na kuahidi tume itasimamia uchaguzi huo kwa misingi ya sheria na haki huku akivitaka vyama vya siasa vishikiane na tume ambayo haina nia wala mpango wa kuweka vizuizi kwa vyama vya siasa.
Nao baadhi ya wawakilishi wa vyama vya siasa ambavyo vitashiriki uchaguzi huo mdogo akiwemo Salma Amour wa ADC na Rashid Mchenga wa ADA, TADEA wamesema wameridhika na maandalizi ingawa wameshuri kasoro kadhaa za kutatuliwa.
Wapiga kura 9225 wanatarajiwa kupiga kura kuchagua mbunge January 22 mwakani baada ya jimbo hilo kuwawazi kutoakna na kifo cha aliyekuwa mbunge marehemu Hafidh Tahir huku baadhi ya vyama vitakavoshiriki ni pamoja na CCM, CUF, ADA, TADEA, CHAUMA, ADC na AFP.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT