Mpaka sasa inaelezwa kuwa tayari wanyama takribani laki moja nchini Iran wamepewa namba za usajili huku wengine 35,000 wakipangwa kusajiliwa kabla ya mwaka huu kumalizika, na sababu kubwa ya kufanya hivyo imetajwa kuwa kuongezeka kwa matukio ya ajali za barabarani.
Maafisa wa usalama nchini Iran wameanza kutekeleza sheria hiyo kwa
majaribio kwenye miji ya Sistan na Baluchestan ambayo iko mpakani mwa
Afghanistan na Pakistan ambako kumekuwa na matukio ya uharibifu wa mali
na ajali za mara kwa mara.
Mohammad-Sharif Khaleqinia, ambaye ni katibu mkuu wa Central Task Force
ameuambia mtandao wa IRNA: “Tunatarajia kutoa namba za usajili kwa
wanyama aina ya Ngamia wapatao 35,000 mpaka kufikia mwisho wa mwaka huu,
lengo letu ni kutaka kutambua mmiliki halali wa wanyama hawa”.
Kwa mujibu wa IFP News, lengo lingine la serikali ya Iran ni kuwafanya
wananchi watimize majukumu yao ya kutunza wanyama wanaowafuga ikiwa ni
pamoja na kupunguza au kuondoa kabisa wanyama wanaozurula mitaani na
kusababisha usumbufu.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT