“Hao wanaosema mimi sio mwana hip hop nipeleke nao kwenye show moja, hao
walionitoa kwenye list ya hip hop. Tena ninachokuomba waandalie show
yao Leaders waweke 16, niandalie show yangu Escape 1 peke yangu.
Nakuambia wakipata watu kweli hip hop yao ina nguvu. Wote unaowasikiaga
waandika, wanakesha, wanatweet ‘Nay si mwanahiphop’ wajikusanye kwenye
show yao moja halafu mimi nipige pale upande wa pili halafu tuone nani
atapata watu,” Nay aliiambia 255 kupitia kipindi cha XXL cha Clouds FM.
“Wewe unakesha unanitukana kwenye mtandao wakati mimi nikiamua asubuhi
naenda kununua gari mpya, nikiamua naenda kununua kibanda chenu kile cha
familia mimi ninakinunua halafu wewe unaenda kukaa unanitukana kwenye
mitandao, siwezi kukasirika,” amesisitiza Nay wa Mitego
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT