Kamanda wa kikosi cha askari wa usalama barabarani wa Kanda Maalum ya
Dar es salaam Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Awadhi Haji akiongea na
madereva wa daladala mapema asubuhi leo jijini humo baada ya kukamata
baadhi yao wakiendesha magari wakiwa wamelewa. ACP Haji amewataka
madereva hao na waendesha vyombo vya moto wengine kujiepusha na jinai
hiyo ya kuendesha gari wakiwa wamelewa kwani ni hatari kwao binafsi na
kwa watumiaji wa barabara. Amesema zoezi hilo la ukaguzi wa madereva
wanaofanya kazi wakiwa wamelewa ni endelevu na kwamba atakayepatikana
atachukuliwa sheria mara moja bila simile.
Mmoja wa madereva wa daladala akipimwa pumzi kuona kama amelewa ama la. Madereva kadhaa walikutwa wamelewa na kuchukulia hatua.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT