Kwa mujibu wa Mkuu wa Idara ya Habari wa Chadema, Tumaini Makene, ujumbe huo unaowahusisha mwanasheria mkuu wa chama, Tundu Lissu na mkurugenzi wa mambo ya nje na mawasiliano, John Mrema utafika katika nchi za Ujerumani, Uingereza na Ubelgiji ambako ni Makao Makuu ya Jumuiya ya Ulaya.
Akiandika katika ukurasa wake wa Twitter, Mbowe amesema, “Nikiwa London, pamoja na ujumbe huo, nitakutana na viongozi mbalimbali wa Serikali, wabunge, ujumbe maalumu wa Jumuiya ya Madola na wawakilishi wa taasisi mbalimbali za kimataifa.”
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT