Mahakama Kuu yafuta kesi ya madai dhidi ya Askofu Kakobe kwa kukosa mashiko | Bepari Classic
Breaking News
Loading...

Ijumaa, 2 Desemba 2016

Mahakama Kuu yafuta kesi ya madai dhidi ya Askofu Kakobe kwa kukosa mashiko

https://i.ytimg.com/vi/C-VGv6hv_FY/maxresdefault.jpgJuzi, Alhamisi 1.12.2016, Jaji Mwandambo wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Dar-Es-Salaam; alifuta kesi ya madai Na.79 ya mwaka 2011 dhidi ya Askofu Mkuu Zachary Kakobe wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), kwa kuona kwamba haina mashiko. Wadai katika kesi hiyo walikuwa watatu, Dezydelius Patrick, Angelo Mutasingwa, na Benedict Kaduma, ambao hapo zamani walikuwa Wachungaji wa Kanisa hilo. Katika kesi hiyo, wadai hao, pamoja na mambo mengine, walidai kwamba Askofu Kakobe alifanya ubadhirifu wa zaidi ya shilingi 14 bilioni.

Katika utetezi, Miriam Majamba ambaye ndiye alikuwa Wakili wa Askofu Kakobe, aliwasilisha vielelezo na kueleza kwamba, Bodi ya Wadhamini ya Kanisa hilo la FGBF, iliwafukuza wadai hao, katika Uchungaji na ushirika wa Kanisa hilo, mwaka 2010. Dezydelius alifukuzwa tarehe 10.9.2010, kutokana na matukio mengi ya utapeli na ubadhirifu, katika Kanisa la FGBF MAFINGA, alilokuwa akiliongoza, na pia utapeli alioufanya kwa waumini wa Kanisa la FGBF Dar-Es-Salaam, Wynn-Jones Kapaliswa na Rhodius Nsaro, aliowatapeli zaidi ya shilingi 34 milioni. Angelo aliyekuwa Mchungaji wa Kanisa la FGBF NZEGA, alifukuzwa Uchungaji, tarehe 6.7.2010, kutokana na ukosefu wa maadili, na vilevile Benedict aliyekuwa Mchungaji wa Kanisa la FGBF BABATI, alifukuzwa Uchungaji, tarehe 23.3.2010, kwa ukosefu wa maadili. Baada ya Wachungaji hao kufukuzwa katika Kanisa hilo, walishirikiana na kupanga mkakati wa kumgeuzia kibao Askofu Kakobe, kwa kutunga madai ya uongo dhidi yake, ili kumchafua; na hatimaye kufungua kesi hiyo ya madai tarehe 26.5.2011.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT