‘Kwanini mpaka sasa kuna kesi 1 tu Mahakama ya Mafisadi’ – Dr. Mwakyembe | Bepari Classic
Breaking News
Loading...

Jumatatu, 19 Desemba 2016

‘Kwanini mpaka sasa kuna kesi 1 tu Mahakama ya Mafisadi’ – Dr. Mwakyembe

Leo December 19 2016 Waziri wa sheria na katiba Dr. Harrison Mwakyembe alikwenda kwenye ofisi ya mkuu wa mkoa Dar es salaam Paul Makonda leo ambao kwa pamoja wametangaza mipango mipya ya kuwasaidia Wananchi wa Dar es salaam kisheria.

Pamoja na mambo mengine waziri Mwakyembe ameeleza jitihada mbalimbali ambazo wizara yake imekuwa ikizifanya ikiwemo uanzishwaji wa mahakama ya makosa ya rushwa na uhujumu uchumi ambayo ilianza kufanya kazi mwezi July na mpaka sasa ni kesi moja tu ambayo imesikilizwa kwenye mahakama hiyo, Waziri Mwakyembe amelizungumzia hilo….

‘Mahakama imeshaanza kufanya kazi lakini baadhi wanahoji kuwa walitegemea kuwe na kesi nyingi toka mwezi july ila tumekuja kubaini kwamba uchache wa kesi ndio mafanikio makubwa ya hatua ya kisheria tuliyochukua, kwa sababu sasa hivi wale waliozoea kupora pesa wamerudi nyuma ya kile kiwango tulichokuwa tumekiweka’
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT