Uchina inaona Taiwan kuwa ni jimbo lake lilojitenga.
Msemaji wa wizara alisema, Uchina ni moja, na ndio msingi wa kisiasa katika uhusiano baina ya Marekani na Uchina.
Mazungumzo ya simu baina ya Bwana Trump na Rais wa Taiwan, Tsai Ing-wen, yamevunja msimamo wa kidiplomasia kwa Marekani.
Ofisi ya rais wa Taiwan ilitoa picha ikionyesha Rais Tsai Ing-we akiongea kwa simu na Trump
Hapo awali, waziri wa mambo ya nchi za nje wa Uchina, Wang Yi, alisema
mazungumzo hayo ya simu ni "ujanja wa Taiwan usiokuwa na maana".
Mwandishi wa BBC anasema ikiwa simu hiyo ni ishara ya mabadiliko ya sera
za Marekani kuhusu Taiwan, basi Uchina itajibu kwa hasira.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT