Chelsea wakomba tuzo tatu za ligi kuu novemba...haijawahi kutokea! | Bepari Classic
Breaking News
Loading...

Jumamosi, 10 Desemba 2016

Chelsea wakomba tuzo tatu za ligi kuu novemba...haijawahi kutokea!

Kutoka kulia Costa, Conte na Pedro wakiwa  na tuzo zao Uwanja wa mazoezi wa Cobham leo baada ya kukabidhiwa

KITENDO cha Chelsea kupaa kileleni mwa Ligi Kuu ya England kimeleta faida kubwa, kwa klabu hiyo kushinda tuzo tatu za mwezi Novemba.

Diego Costa amekuwa Mchezaji Bora wa Mwezi Novemba, wakati Antonio Conte amekuwa Kocha Bora na Pedro ameshinda tuzo ya Bao Bora la Mwezi alilofunga katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Tottenham.

Tuzo hizo zinazotokana na kura za mashabiki na wataalamu, zinakuja mwezi mmoja baada ya Conte na mchezaji wake nyota, Eden Hazard kushinda tuzo za Mchezaji Bora na Kocha Bora kwa mwezi Oktoba.

Hii inakuwa mara ya kwanza tuzo zote tatu zinakwenda kwa klabu moja na inafuatia Chelsea kushinda mechi zote tatu za Ligi Kuu mwezi Novemba - wakiichapa Everton 5-0 kabla ya kuzifunga na Middlesbrough na mahasimu wao wa London, Tottenham.

Waliendeleza wimbi lao la ushindi la Novemba na kwa kushinda mchezo wao wa kwanza wa Desemba wakitoka nyuma na kuifunga Manchester City 3-1 Uwanja wa Etihad.

Costa, ambaye alifunga mabao mawili katika mechi tatu za Chelsea Novemba, alisema baada ya kupokea tuzo yake: "Mambo yanakwenda vizuri kwa sasa. Timu inafanya vizuri na hii inaonyesha kwamba mambo yananinyookea,".

MATOKEO YA CHELSEA MWEZI NOVEMBA 

Chelsea 5-0 Everton
Middlesbrough 0-1 Chelsea
Chelsea 2-1 Tottenham 
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT