CCM yashinda Umeya Kigamboni | Bepari Classic
Breaking News
Loading...

Jumamosi, 17 Desemba 2016

CCM yashinda Umeya Kigamboni

Dar es Salaam. Diwani wa Kata ya Pemba Mnazi (CCM), Maabadi Hoja ameshinda umeya wa Halmashauri mpya ya Kigamboni baada ya kupata kura tisa dhidi ya tano za Celestine Maufi wa Chadema.

Uchaguzi huo umefanyika leo (Jumamosi )katika  Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Julisu Nyerere kilichopo Kigamboni.

Mwenyekiti wa uchaguzi huo, Upendo Wera amesema jumla ya kura zilizopigwa ni 15 na moja iliharibika.

Wera ambaye ni Katibu Tawala wa Kigamboni, amesema nafasi ya naibu meya imekwenda kwa Amin Sambo kutoka CCM aliyemshinda Ernest Mafimbo wa CUF chini ya Ukawa.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT