Wasira: Uzee sio sababu ya kukubali kushindwa kirahisi | Bepari Classic
Breaking News
Loading...

Jumamosi, 19 Novemba 2016

Wasira: Uzee sio sababu ya kukubali kushindwa kirahisi

Dar es Salaam. Waziri wa muda mrefu na mbunge wa zamani wa Bunda, Steven Wasira amewajibu wanaodai kwamba amelazimika kustaafu siasa baada ya mpinzani wake, Ester Bulaya kuwashinda wapigakura wanne waliokuwa wakipinga ushindi wake wa ubunge wa Bunda Mjini na kusema hajastaafu na uzee haumzuii mtu kudai haki yake.

Juzi, Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza ilimpa ushindi Bulaya katika kesi ya uchaguzi hali iliyotafsiriwa na wadadisi wa kisiasa kwamba huo ndiyo ulikuwa mwisho wa kisiasa wa Wasira.

Lakini jana, Wasira alipopigiwa simu na waandishi wetu kuelezea hatima yake ya kisiasa baada ya kesi hiyo, alisema wanaodai kuwa anatakiwa kustaafu siasa kwa sababu ni mzee hawana budi kuangalia kauli zao kwa sababu wapo wazee wengi anaowafahamu kwa majina na bado wapo madarakani.

“Suala la kusema nimestaafu siasa silijui na sijawahi kusema. Kesi hiyo inahusiana nini na siasa? Wapigakura wameona kuwa uchaguzi haukuwa huru na haki. Hakuna uhusiano na uhusiano uliopo ni kwa sababu mimi ni shahidi na mimi niligombea,” alisema na kuongeza:

“Nataka wanipe ‘definition’ (maana) ya kustaafu siasa. Je, ni kunyamaza, nisitoe maoni. Mbona wapo watu walikuwa wanasiasa na bado wanatoa maoni ya kisiasa tena yenye manufaa makubwa?”
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT