Dar es Salaam.
Kama ulikopa Twiga Bancorp, bado hujasalimika inabidi tu uwasilishe fedha hizo, kwani Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imesema inaendelea na uchunguzi wa watu waliokopa ili iwabane.
Kama ulikopa Twiga Bancorp, bado hujasalimika inabidi tu uwasilishe fedha hizo, kwani Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imesema inaendelea na uchunguzi wa watu waliokopa ili iwabane.
Benki hiyo imefilisika na kuwekwa chini ya usimamisi wa BoT baada ya
kubainika kuwa mtaji uko katika hali mbaya kiasi cha kuweka hatarini
fedha za wateja.
Gavana wa BoT, Profesa Benno Ndullu alisema wiki iliyopita kuwa benki
hiyo ilikuwa na mtaji hasi wa Sh21 bilioni baada ya kuanza na mtaji wa
Sh7.5 bilioni unaokubalika kisheria.
Alipoulizwa kwa njia ya simu kuhusu orodha ya wakopaji wa benki hiyo,
msimamizi wa benki wa BoT, Kennedy Nyoni amesema kwa sasa bado
wanachunguza waliokopa na ripoti itatolewa wiki ijayo.
“Tulichofanya ni kuchukua usimamizi wa hiyo benki na kumweka mtu wetu
pale. Sheria ya Benki inatoa siku 90 za uchunguzi, lakini hadi wiki
ijayo tutakuwa tumepata taarifa. Hata leo (jana) tuko ofisini
tunaendelea na uchunguzi,” amesema Nyoni.
Akizungumza na waandishi wakati wa kutangaza kufilisika kwa benki hiyo,
Gavana Ndulu alisema bado benki hiyo inazo mali zinazofikia Sh90 bilioni
na Sh9 bilioni kati ya hizo haziko vizuri.
Alisema wametumia kifungu namba 56(1) (g)(I) na 56(2) (a-d) cha Sheria
ya Benki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006, kuiweka Twiga chini ya
usimamizi wa BoT.
Twiga Bancorp ilianzishwa mwaka 1992 ikiwa chini ya Benki ya Taifa ya
Biashara (NBC), na mwaka 1998 ikabadilishwa na kuruhusiwa kufanya kazi
zote za kibenki isipokuwa za kibenki isipokuwa kupokea au kuchukua fedha
za akaunti za kawaida.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT