Habari yako rafiki yangu? Bila shaka unaendelea vyema na shughuli zako. Kwa upande wangu niko vyema, nashukuru Mungu sana kwa neema zake juu yangu. Leo nitazungumzia kuhusu mitandao ya kijamii, kwa sababu watu wengi wanatumia zaidi ya saa moja wakiwa kwenye mitandao ya kijamii. Si jambo la kushangaza sana lakini kutakuwa na tatizo tu kwa namna moja au nyingine.
Nikiri mitandao ya kijamii imefanya mapinduzi makubwa katika tasnia ya mawasiliano na habari na imekuwa na nguvu kubwa kuliko hata vyombo rasmi vya habari. Mitandao hii itaendelea kuwa na faida nyingi na kubwa sana kwa jamii. Ugunduzi wa mitandao huu umeendelea kutumika kama jukwaa la kupashana habari, kubadilishana maarifa, jukwaa la matangazo nakadhalika.
Mitandao ya kijami inaendelea kuboresha maisha ya watu waliojitambua na kujua nini cha kufanya kwenye mitandao ya kijamii. Lakini kwa walio wengi mitandao ya kijamii inaendelea kuwa kaburi la maono ya watu bila wao kujua; na yote haya yanatokana na watu wengi kutojua nini cha kufanya katika mitandao hii. Hii mitandao ina nguvu kubwa sana kuharibu maono yako na kukufanya kuwa maskini wakudumu.
Nimeandika makala hii ili nikusaidie kutoka kwenye mtego huu. Nia na madhumu ni kukusaidia kutumia mitandao hii katika hali bora yenye tija katika maisha yako. Nafahamu kila mtu ana maono ya kufanikisha kitu fulani hapa duniani, na pia maono hayo ndio kusudi la kuumbwa kwako hapa duniani. Sasa kama hutochukua hatua stahiki juu ya mitandao ya kijamii ni wazi hutafikia maono yako kabisa.
Ebu tuone ni kwa namna gani unajeruhi maono yako kupitia mitandao ya kijamii:-
Moja, Taarifa ni Nguvu. Taarifa ni nguvu katika muktadha wa kubadili mtizamo na tabia ya mwanadamu. Taarifa unazozipata na kuuruhusu ubongo wako kuzichakata zina nafasi kubwa ya kutwaliwa na kuwa mtizamo wako, na hili litategemea sana kiwango cha upokeaji wa taarifa husika. Habari nyingi kwenye mitandao ya kijamii ni hasi, ni hasi kwa sababu kiasili binadamu tunapenda habari hasi sana.
Kupitia habari hasi za kwenye mitandao ya kijamii unazidi kujenga hofu ya maisha, wasiwasi, lawama na ubishi, tabia ambazo ni kikwazo. Kama utaendelea kupokea taarifa hasi za kwenye mitandao ya kijamii kwa zaidi ya saa kila siku ni wazi utajenga mtizamo hasi ambao utakuwa kikwazo kikubwa katika safari yako ya mafanikio.
Ukijenga utamaduni wa kutembelea mtandao huu kila siku muda si mrefu unakuwa tajiri wa mali, maarifa na afya. Kazi kwako!
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT