Upo
usemi kwamba fahari wawili hawakai zizi moja, ndicho kinaonekana kutokea
kati ya mastaa wakubwa wa Bongo Flava nchini, Diamond Platnumz na Ommy
Dimpoz ambao waliwahi kuwa marafiki zamani, lakini sasa wamethibitisha
wazi kuwa hawako poa kama mwanzo.
Kupitia
Interview iliyofanywa ndani ya show ya XXL kupitia Clouds FM jana
November 23, 2016, Diamond Platnumz alifungua kifua na kueleza mambo
mengi sana juu ya tofauti yake yeye na Ommy Dimpoz ikiwemo lakini
hakikuwekwa wazi sana chanzo cha kutofautiana kwao.
“Hivi
jamani kweli mimi nigombane na Ommy Dimpoz kwasababu ya Wema Sepetu
kweli? Siwezi kufanya hivyo. Mimi nafikiri tusilizungumzie nadhani wenye
macho wameshanielewa kama hawajaelewa tangu jana waje kuelewa leo?
watakuwa washaelewa. Dozen mimi naamua kumsitiri mwenzangu.” – Diamond
Leo
November 24, 2016 Ommy Dimpoz amepiga story na XXL ya Clouds FM pia,
ambapo ameeleza kwa upande wake amepokeaje maelezo ya Diamond pamoja na
ufafanuzi kuhusu ukaribu wake na watu ambao Diamond ameshatofautiana nao
pamoja na kufanya kazi na Wema Sepetu.
“Mimi
kwenda kushoot video ya Wanjera ndio ilikuwa sababu ya kutofautiana na
Diamond, unajua mimi na Wema ni washkaji tangu hajaanza kuwa mpenzi wa
Diamond, mimi nilimuweka Wema kwababu ana mashabiki wengi na nilitaka
impact ya kazi yangu, mimi pia sijawahi kudate na Wema” – Ommy Dimpoz
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT