Wizara
ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imekanusha taarifa zilizoenea ya kuwa,
Waziri wa Elimu Prof. Ndalichako amezuia wanafunzi wenye Stashahada
(Diploma) kujiunga na masomo ya Shahada (Degree) katika vyuo vikuu.
Kwa mujibu
wa taarifa iliyotolewa na Naibu Waziri wa Elimu, Mhandisi Stella
Manyanya amesema kuwa, katazo lililotolewa na Waziri Prof. Ndalichako
siku ya mahafali ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania linawahusi wale tu
wanaosoma Foundation Courses ili kuweza kujipatia sifa za kujiunga na
chuo kikuu.
Taarifa
imeeleza kuwa awali wanafunzi ambao walifeli kidato cha nne walikuwa
wakisoma Foundation Courses katika vyuo mbalimbali na kisha kujipatia
sifa za kujiunga na chuo kikuu kitu ambacho waziri alisema sasa
hakitakuwepo tena.
Utaratibu
huu ulikuwa ukitumika zaidi katika Chuo Kikuu Huria ambapo wanafunzi
walikuwa wakisoma programu maalum zilizokuwa zikiwapa sifa ya kusoma
Shahada.
“Kilichojitokeza
ni kuna taarifa zinasambaa kwamba kuanzia sasa wanafunzi watakaoenda
chuo kikuu ni wale ambao tu wamepitia form six sasa hiyo taarifa imeleta
presha kubwa, nimekuja hapa sio kukataa tamko hilo hapana nimekuja
kulitolea ufafanuzi.” – Naibu Waziri Eng. Stella Manyanya
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT