Tetemeko la ardhi mkoani Tanga lavunja majengo ya shule ya msingi Kange. | Bepari Classic
Breaking News
Loading...

Jumamosi, 26 Novemba 2016

Tetemeko la ardhi mkoani Tanga lavunja majengo ya shule ya msingi Kange.

Halmashauri ya jiji la Tanga inakusudia kuvunja majengo ya shule ya msingi Kange kufuatia tetemeko la ardhi kuvunja baadhi ya kuta za madarasa na ofisi za walimu na kutenga nyufa kubwa hatua ambayo inaweza kusababisha maafa kwa walimu na wanafunzi wa shule hiyo.

Akizungumza katika shule hiyo wakati kampuni ya saruji Tanga ilipokuwa ikimkabidhi mkuu wa wilaya ya Tanga madarasa mawili na vyoo baada ya tetemeko la ardhi kuharibu vibaya madarasa, mkurugenzi wa halmashauri ya jiji la Tanga Daud Mayeji amesema wameanza kuwashirikisha wataalam wa hali ya hewa pamoja na jeshi la anga kutoa taifa la Marekani ili kukabiliana changamoto hiyo.

Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kange Deborah Mnzavar amesema kipindi cha upepo wanalazimika kuwaruhusu wanafunzi kurudi majumbani kwa kuhofia majengo ya shule hiyo yenye nyufa kubwa kuangukia wanafunzi na walimu na kusababisha maafa yanayoweza kuzuilika.

Kufuatia hatua hiyo kamati ya ulinzi na usalama iliyoshiriki katika hafla ya kukabidhiwa vyumba viwili vya madarasa na vyoo ili kuwapunguzia changamoto wanafunzi hao, mwenyekiti wake ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa ameshukuru kwa msaada huo lakini amemwagiza mkurugenzi wa halmashauri kutafuta walimu wa wanafunzi wenye mahitaji maalum ili waweze kunufaika kimasomo.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT