Faida hiyo iliyopatikana kwa mara ya kwanza baada ya kipindi kirefu, inatokana na shirika hilo kuwa katika hali nzuri, baada ya kuwa limetoka katika kupata hasara ghafi ya Sh bilioni 496 kwa mwaka 2013, huku upotevu wa umeme ukipungua kutoka asilimia 21 mwaka 2012 hadi asilimia 17 mwaka huu.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Felchesmi Mramba amesema hayo hivi karibuni kuwa rasilimali zake zimeongezeka kutoka Sh trilioni 3.8 mwaka 2013 hadi trilioni 5.2 mwaka 2014 ikiwa ni ongezeko la asilimia 36.8.
Alisema si kweli kuwa sekta ya umeme ina hali mbaya kwani ni nzuri na yenye maendeleo kwani kipindi kama hiki mwaka jana kulikuwa na upungufu wa megawati 300 za umeme na kulikuwa na mgawo lakini sasa hakuna upungufu wa umeme wakati mahitaji yakiongezeka kutoka megawati 1000 kwa wakati huo hadi 1041.
Mramba amesema kuhusu matatizo ya bili za wateja kwa kutumia mfumo wa luku tayari asilimia 96 ya wateja wote nchini wanatumia mita hizo hivyo kuondoa malalamiko ya bili na asilimia nne iliyobaki iliyo katika mikoa ya Mbeya, Kilimanjaro, Arusha na Mwanza itakuwa imebadilishwa kuwa na luku ifikapo Machi, mwakani.
Amesema nchi itakuwa ya kwanza kwa wateja wake wote kutumia mita za luku huku mfumo wake umeboreshwa na tayari asilimia 41 ya kukatika katika kwa umeme imeondolewa na wanatarajia ifikapo Februari mwakani, utakuwa ukikatika kwa nadra.
Kuhusu kupandishwa kwa bei ya umeme, Mramba amesema imepeleka mapendekezo kwa mdhibiti kama sheria inavyowataka ili bei iangaliwe na gharama halisi, bei waliyoomba haitawaathiri wateja wadogo wa kawaida bali makundi ya kibiashara.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT