Mkurugenzi wa idara ya Afrika wa Wizara ya Mambo ya nje na ushirikiano
wa frika Mashariki, Balozi Samweli Shelukindo akizungumza na waandishi
wa Habari
RAIS wa Zambia Edgar Lungu anataraji kuwasili nchini kwa ziara ya
siku tatu nchini Tanzania kwa mwaliko wa Rais John Pombe Magufuli
kuanzia Novemba 27 mpaka 29.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Waziri wa Mambo
ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Augustine Mahiga,
amesema ziara hiyo ambayo inatarajia kukuza na kuimarisha uhusiano
uliopo kati ya nchi hizi mbili.
“katika ziara hii Rais wa Zambia atatembelea Bandari ya Dar es Salaam,
Reli ya Tazara na mradi wa bomba la mafuta la TAZAMA amabalo limetoka
hapa nchini mpaka Zambia” amesema Balozi Mahiga.
Amemaliza kwa kusema kuwa ni vyema watu wakaanza kuiona kariakoo kama
sehemu ambayo inasaidia kukuza mahusiano yetu kati ya Tanzania na Zambia
kwa kuwezesha wanawake zaidi 1000 ambao hufika sokoni hapo kila siku.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT