Jeshi la Polisi Zanzibar limemfukuza kazi askari wake baada ya kukamatwa
akimfanyia mtihani mwanafunzi wa kidato cha nne kinyume na sheria huku
kukiwa na taarifa za baadhi ya wanafunzi kukamatwa kwa kuhusika na
kukutwa na mitihani ya kidato cha nne.
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa mjini Magharibi kamishna msaidizi
mwandamizi SACP Hassan Nassir amethibitisha kwa jeshi la polisi
kumfukuza kazi askari huyo F9592 Hassan Haji Jecha ambaye kwa sasa ni
mwanafunzi wa chuo kikuu akichuka digrii ya pili amekutwa akimfanyia
mtihani mwanafunzi Said Haji kitendo ambacho ni aibu.
Katika hatua nyengine ITV iliwakuta wazee waliojazana nje ya makao makuu
ya polisi mkoa wa mjini Magharibi wakilalamika watoto wao kuwekwa ndani
bila ya taarifa kwa madai ya kuvujisha mitihani ya kidato cha nne
kupitia mitandao ya simu wakiongea na ITV baadhi ya wazee wa watoto hoa
wameshangazwa na uamuzi wa polisi kutoa taarifa yeyote wanafunzi hao
idadi yao haijajulikana wamekamatwa kutoka sehemu mbalimbali huku pakiwa
na taarifa ya baadhi ya wataalam kutoka Dar es Salaam wamewasili
Zanzibar kufuatia suala hilo.
Hata hivyo wakati wazee hao wanawalilia watoto wao wakiwa ndani ya jengo
la polisi kamanda Hassan Nassiri amepinga madai hayo akidai hana
taarifa za kuwepo kwa tatizo hilo la kukamatwa wanafunzi kwa shtuma za
mitihani hiyo ya kidato cha nne.
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT