Swala la nini kinapaswa kuwa cha kwanza kati yamtaji wa fedha na wazo la kibiashara limewatatiza wengi sawa na shairi lile la darasa la tano liliouliza "YAI AU KUKU NANI KATANGULIA?"
- Uhalisia ni kwamba hata fedha yenyewe ni wazo na kimsingi kitu chochote cha kushikika kilitokana na wazo fulani na badae wazo hilo likawekwa katika uhalisia.
Siku moja nilikuwa naongea na watu fulani
nikawaambia kwamba siku zote mtaji fedha hufuata mtaji wazo .Yapo mawazo
ambayo yanakupa mbinu za kupata fedha hivyo basi tatizo kubwa tusiseme
ni mtaji fedha lakini wengi tuna tatizo la kukosa mtaji wazo.
- Ukweli ni kwamba watu wengi hatuna mawazo .Kwa mujibu wa mwandishi wa vitabu,mhamasishaji na mwanzilishi wa makanisa ya winners chappel Pator David Oyedepo anasema “``` 5% ya watu wote duniani ndio wenye mawazo, 15% ya watu wanadhani kuwa wanawaza kumbe hawawazi na 80% ya watu wote duniani wanakufa bila kuwaza”(hii ni hatari).```
Napoleon Hill aliwahi kuuliza swali hili ```"if
you get a million dollar what will you do???"```. Napoleon Hill
alitambua kuwa binadamu wengi wanalamika hawana fedha huku wakiwa hawana
mawazo ya nini watafanya baada ya kupata fedha .Wewe ni shahidi umekuwa
ukipata pesa mara ngapi na umezifanyia nini??(unajua mwenyewe).
Watu
wengi wana fedha lakini hawana mawazo sasa kwako wewe hii ni fursa ya
kutumia mtaji wazo kupata hizi fedha ambazo hazina kazi zimekaa tu
.Shida wengi hatutaki kuumiza vichwa na kuzalisha mawazo yenye tija
*(productive ideas)*.Kama wewe una sh laki moja na unahitaji kuanza
biashara ya laki sita na huna fedha hiyo kwanini usiungane na marafiki
wazuri 6 ulionao wenye uwezo wa kupata laki moja kwa mwezi mkafanya
mchezo na ukapata hiyo pesa kiulaini???(umekosa mawazo siyo mtaji).
- Kuna watu hapa mjini ni *madalali* wa mambo lukuki na wanapata hela sana bila kutumia hata chembe ya shillingi .Fikiria dalali anapangisha watu watano au kumi kwa mwezi anapata sh ngapi ?? bado dalali huyu huyu yuko kwenye viwanja, kumbi n.k .Mtu huyu anapata pesa nyingi .
Kuwa dalali siyo kwamba hujasoma , acha mawazo
potofu .Dalali ni *Third part* anayekurahisishia kupata huduma uitakayo
haraka hata wewe unaweza kuamua kuwa dalali na ukaendelea na maisha
(tumekuwa vipofu)
- Acha kabisa kulalamika kuwa huna mtaji wakati huo una simu ya laki saba na unaweka vifurushi ya elfu moja kila siku na kupanda bodaboda kila siku na hujui kwa mwaka unatumia kiasi kikubwa kiasi gani huku ukisema huna mtaji wa laki mbili kuanzisha biashara
```Akili yako ,Maisha yako```
Ukijenga utamaduni wa kutembelea mtandao huu kila siku muda si mrefu unakuwa tajiri wa mali, maarifa na afya. Kazi kwako!
Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini
0 comments:
POST A COMMENT