Mkuu wa Mkoa Kagera atoa ufafanuzi wa makusanyo ya fedha za maafa. | Bepari Classic
Breaking News
Loading...

Jumamosi, 19 Novemba 2016

Mkuu wa Mkoa Kagera atoa ufafanuzi wa makusanyo ya fedha za maafa.

Mkuu wa mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Mstapha Kijuu ametoa ufafanuzi wa kukusanya fedha inayoendelea kutolewa na wadau mbalimbali yakiwemo mashirika ya kimataifa,nchi rafiki,taasisi za kiserikali na zile za kibinafsi kwa ajili ya kuyakabili madhara ya tetemeko la ardhi lililotokea mkoani humo ili kuondoa utata wa matumizi ya fedha hiyo.

Mkuu huyo wa mkoa ametoa ufafanuzi huyo wakati wa kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa wa Kagera,baada ya Mstahiki Meya wa Manispaa ya Bukoba Chief Kalumuna kuonyesha kutoridhishwa na kiasi cha fedha cha zaidi ya shilingi bilioni 5.4 kilichoko kwenye akaunti ya maafa Kagera kilichotajwa kuwa ndicho kilichochangwa na wadau kwa ajili ya waathirika wa tetemeko, mkuu huyo wa mkoa amesema fedha ya kuyakabili maafa ya tetemeko inakusanywa kupitia akaunti ya maafa iliyofunguliwa mkoani Kagera na fedha nyingine zinazotolewa zinapokelewa na kitengo cha maafa cha Ofisi ya Waziri Mkuu.

Kwa upande wake,Mbunge wa Jimbo la Karagwe,Innocent Bashungwa ameiomba serikali itoe ruzuku kwenye ununuzi wa vifaa ya ujenzi ili waathirika wa tetemeko waweze kununua vifaa hivyo kwa bei rahisi,naye,Mbunge wa Jimbo la Muleba Kusini Profesa Anna Tibaijuka ameiomba kamati ya maafa ya mkoa wa Kagera irasimishe majukumu ya kushughulikia madhara ya tetemeko kwa kamati za wilaya ili misaada inayotolewa iwafikie wananchi kwa wakati.


Download Video and Put Comment
Toa Maoni Hapa Chini

google+

linkedin

0 comments:

POST A COMMENT